Kwa kuwa utalii ni sekta ambayo inachangia sehemu kubwa ya pato la taifa wadau wengi wa utalii wamekuwa wakikerwa na kusikitishwa na mambo mabaya wanayofanyiwa wataalii wanaotembelea visiwa vyetu vya Zanzibar, kwa mfano kukabwa, kuibiwa, kupigwa na mambo mengineo ambayo ni kinyume na utamaduni wa Kizanzibari.

Licha ya mambo hayo pia wadau hao wameonyesha kukerwa na kusikotishwa zaidi na upande wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kwa aidha kuchukuwa hatochukua hatua juu ya masuala hayo ama kutojihusisha kabisa katika kufanya Indhari ili mambo hayo yasitokee, ambapo yakiendelea kutokea ni kitisho kinachoweza kuchangia kushika kwa idadi ya watalii wanaotembea Zanzibar kwa kuhofia usalama wao na Mali zao.

Mzee Ameir bin Ameir bin Soud wa kijiji cha Bwejuu Kusini mwa Kisiwa cha Unguja, ni miongoni mwa wadau wa utalii na historia ya Zanzibar pamoja na Tanzania ni miongoni mwa wadau wanaosikitishwa na hali kama hii juu suala zima LA usalama wa watalii.

Na Ali Mohammed
Na Ali Mohammed

Akichangia mada ya Utalii Zanzibar katika kituo cha Redio ya Chuchu FM, Mzee Ameir alisema kwamba katika Mkoa wa Kusini kuna Mkondo Mkubwa wa Bahari wenye kina cha futi 12 za mtu mzima, miaka yote watalii hufa katika mkondo huo, lakini hadi sasa hakuna indhari yeyote inayotolewa kwa upande wa hoteli za ukanda huo na hata serikali, na kusisitiza kwamba hilo ni kosa.

“Kubwa kuliko yote ni pale yanapotokea maafa kwa watalii serikali haiwajibiki kutoa taarifa kwa wananchi licha ya kuepo sheria inayowapa wananchi haki ya kupata habari.

“Leo ya tatu au ya nne na hata Chuchu (redio station) wanayotaarifa kwamba watalii katika sehemu ya dongwe Msuakini, watalii walivamiwa na wizi na majambazi kwa kutumia silaha, lakini Serikali iko kimya (SMZ), Jeshi la Polisi liko kimya, tume ya utalii (Kamisheni) iko kimya, wakati ikijua nchi za mwenzetu zote hata Tanzania bara likitokea lolote akiguswa mtalii serikali ya Tanzania bara (SMT) hua inatoa taarifa kwa watu wote wawe ” Attention”, ili ipatikane ile faida ya watalii kwa wote.

“Lakini Zanzibar Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko kimya haijali maisha ya watalii inajali mapato tu, hilo ni tatizo litapelekea sekta hii kuvunjika.

“Tunatoa indhari serikali (SMZ) lazima ithamini wageni wote wanaoingia katika visiwa hivi, kwa sababu imekubali kwa ridhaa watalii watoke kwao waingie visiwa hivi kwa Salama na amanina arudi kwao kwa amani na hili tunaiambia serikali ikifurahi, ikichukiwa lakini tunaieleza lazima ithamini usalama wa wageni wetu” alisema Mzee Ameir bin Ameir Bin Soud.

Licha ya matukio hayo, yapo pia matukio ya kuporwa kwa wageni katika fukwe za ukanda wa Kowengwa – Pwani mchangani, ambapo wahudumu wa ndege walikuwa wamejipumzisha katika fukwe za Melia Resort pia waliporwa Paso zao za kusafiria, peza, simu na vitu vyemgine vidogo.

Siku mbili baada ya tuko hili katika ukanda huo huo katika fukwe za Ukumbi wa Starehe unaoitwa Gabi Beach pembezoni kwa hotel hii ya Melia pia watalii walikabwa na kunyanganywa Mali zao ingawa Polisi walibahatika kuwakamata na baadhi ya Mali za watalii hao zilipatikana ingawa fedha walizowanyanganya hazikiweza kupatikana baada ya maharamia hao kueleza kwamba walishazitumia.

Mbali ya matendo hayo ya kiharamia bado kuna malalamiko wanayotoa baadhi ya watalii kuhusiana kodi za ziada kama zile za “Infrastructure Tax” ambayo ni malipo ya ziada mtalii hutakiwa kulipa dola moja kwa mtu pale anapoondoka hoteli nje ya matumizi aliyotumia hotelini hapo, sambamba na hilo watalii pia wamekuwa wakilalamikia jinsi vijana wanaotafuta riski zao katika fukwe zenye hoteli za kitalii “Beach boys”.

” Beach boys” ni watu wanaopendwa sana na baadhi ya watalii ili kiwatembeza sehemu mbali mbali licha ya kuwa hawajarasimishwa na serikali kufanya shughuli hii, lakini kumekuwa na malalamiko kwa wale wageni ambao wamefika Zanzibar kwa ajili yakupumzika na sio kutembea, kwa sababu kuna makundi mawili ya watalii, wapo waliokuja kwa kutembea na kuona na kusema historia na kuna walikuja kwa mapumziko tu.

Hivyo serikali inapaswa kuwaelemisha “Beach Boys” kufanya shughuli zao kwa ustaarabu wakizingatia makundi hayo, ni kheri kutafuta mbinu mbadala ya kushawishi kuliko hii inayotumika sasa ya kiwaita “halo my friend” pindipo wakiwa wamejilaza katika vitanda vya ufukweni “Beach beds” ukizingatia tofauti ya makundi hayo ya watalii niliyoyaeleza, ni kheri waandike mabango wawaonnyeshe watalii zile huduma wazitoazo kuliko kuwapigia kelele kwani kuna wanaofurahi na wanaochukia.

Hivyo naungana na wadau wote wa utalii akiwemo Mzee Ameir Bin Ameir Bin Soud kuiambia serikali kwamba iache tabia ya kuwabeza watalii, na iweke mkakati imara wa kuhakikisha ulinzi wa lazima kwao na malizao ili kufanya sekta hii inadumu na kukua, endapo serikali isipowajibika kwa hili, washindani wetu ambao wanjiimarisha kila uchao watarithi soko letu, nakutuachaa mataani.

 

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.