“Nataka kuwa kama Maalim Seif”

Published on :

Sikumbuki mwezi wala tarehe, lakini mwaka ni 1985. Naukumbuka mwaka huo kwa kuwa nilikuwa darasa la tatu katika skuli yangu ya Pandani. Kinachonifanya niukumbuke mwaka ni hilo darasa lenyewe nililokuwa nikisoma. Chumba chetu kilikuwa upande wa kushoto wa ofisi ya Mwalimu Mkuu, Maalim Nassor Hemed Khamis (Allah amrehemu), na kutokea […]

Kilichomtokea Dk. Shein mjini Moroni na fasili ya kisheria

Published on :

Hivi majuzi, Dk. Ali Mohammed Shein alihudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais wa visiwa vya Comoro zilizofanyika mjini Moroni. Habari zinasema alikwenda huko kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, ambaye ndiye aliyealikwa rasmi. Picha zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zilimuonesha Dk. Shein akiwa amekaa […]

Dk. Shein, Dadi na Msangi, kwani Mungu si Mbora wa kuhukumu?

Published on :

Ni Qur’an ndiyo inayouliza swali hilo katika sura yake ya 95, aya ya 7. Namna ilivyokuwa na miujiza, katika aya ya 4 ya sura hiyo hiyo, Qur’an inaelezea namna Mwenyezi Mungu anavyojisifu kwa kumuumba mwanaadamu kwa umbile lililo bora kabisa, lakini kisha, hapo hapo, inafuatia aya ya 5 inayoonesha nguvu […]

Maalim Seif, mtu aliyekuwa na daima atakayekuwa

Published on :

Picha inayosawiri makala hii niliipiga tarehe 24 Julai 2010, nje ya msikiti wa Ijtimai, Fuoni, magharibi ya kisiwa cha Unguja. Angalia huyo mtoto mkono wa kushoto ambaye anawania kumpa mkono Maalim Seif Sharif Hamad. Nakisia kuwa wakati huo alikuwa na miaka 12 au 13, umri ambao anao mtoto wangu wa […]

Hakuna wa kuizima nyota ya Maalim Seif

Published on :

Majina matatu ya Idri Abdul-wakil Nombe, Seif Sharif Hamad na Salmin Amour Juma ndio yaliojadiliwa na Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM-NEC ili kuteua mmoja wapo kuwa rais mpya atakaemrithi Mzee Ali Hassan Mwinyi. Mzee Idris Abdulwakil Nombe alikuwa wa mwanzo kuomba jina lake liondoshwe mezani kutokana na sababu za […]