Maalim Seif

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kuwa licha ya Dk. Ali Mohamed Shein kujisifu kuwa hatategemea wafadhili wa kimaendeleo, kiongozi huyo aliyeingia madarakani kwa uchaguzi wenye utata hana uwezo wa kuiendesha serikali yake bila ya misaada ya wahisani wa kimataifa.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Hoteli ya Hyat mjini Zanzibar hivi leo (Aprili 10), Maalim Seif, ambaye yeye na chama chake wanaamini ndio washindi halali wa uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana, alisema kwamba serikali iliyopita ambayo chama chake kilikuwa mshirika mdogo ilikuwa na nakisi kubwa ya fedha za matumizi ya kila siku, kiasi cha kwamba wizara kadhaa zilikuwa zinapatiwa chini ya asilimia 30 ya mahitaji halisi.

Katika mkutano huo uliokusudiwa kutoa muelekeo wa CUF baada ya maazimio ya Baraza lake Kuu la Uongozi wiki iliyopita, Maalim Seif alisema chama chake “kitatumia njia za amani na za kidemokrasia kushinikiza ipatikane haki ya Wazanzibari.”

Zaidi sikiliza hapo chini.

https://soundcloud.com/mohammed-k-ghassani/shein-hana-ubavu-wa-kuendesha-serikali-bila-misaada-maalim-seif

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.