Kutokana na hali hiyo kuna kila aina ya uvunjaji wa haki za binadamu unaendelea Zazibar kwa kisingizio cha kudhibiti amani. Kumekuwa na vikundi viovu vikiwavamia wafuasi wa CUF na kuwapiga pamoja na kuwajeruhi, maarufu kwa jina la Mazombi. Jeshi la paolisi, pamoja na kujinadi kwamba wana kila mbinu za kiintelejensia, mpaka leo hii hawajakamata Zombi hata mmoja na wanasema hawawajui na hawapo.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI                                                                                                             17 Machi 2016

Ndugu waandishi wa habari,

Januari 11, 2016, CUF tulitangaza kutoshirirki uchaguzi wa wa marudio wa Zanzibar na huo ndio msimamo wetu na hautabadilika.

Mara baada a kuutanganga umauzi huo tunajua CCM watajitangazia uraisi na utawala wao kama kawaida.Hivi sasa kuna kila jitihada za CCM kwa kuvitumia vyombo vya usalama wanataka wanalazimisha wazanzibar kwenda kupiga kura uchaguzi haramu wa tarehe 20/03/2016 ili kuhalalaisha CCM kujitangaza washindi.

CUF kupitia Katibu Mkuu wa Chama, Maalim Seif Sharif Hamad, alitoa wito ambao tumeendelea kuusisitiza kuwa wananchi wa Zanzibar hasa wafuasi wa CUF waendelee kuwa watulivu. Wafuasi wa CUF wametulia sana na wanaendelea na shughuli zao licha ya kuchokozwa mara kwa mara na CCM pamoja na vyombo vya dola.Ofisi za CUF Pemba na yumba za wafuasi kadhaa zimeendelea kuchomwa moto na watu wanaojiita Mazombi.

Kutokana na hali hiyo kunakila aina ya uvunjaji wa haki za binadamu unaendelea Zazibar kwa kisingizio cha kudhibiti amani ya Zanzibar.
Kumekuwa na vikundi viovu vikiwavamia wafuasi wa CUF na kuwapiga pamoja na kuwajeruhi, maarufu kwa jina la Mazombi. Jeshi la paolisi pamoja na kujinadi kwamba wana kila mbinu za kiintelejensia mpaka leo hii hawajakamata Zombi hata mmoja na wanasema kwamba hao mazombi hawawajui na hawapo.

Lakini la kushangaza kila tukio baya likitokea Zaznzabar wanasingiziwa wafuasi wa CUF.Kila siku wafuasi wa CUF wanakamatwa na mpaka hivi sasa wafuasi wa CUF zaidi ya 60 wamekamatwa wakisingiziwa kuhusika na uvunjifu wa amani.

Viongozi kadhaa wa CUF wameendelea kukamatwa na kuwekwa vizuizini wengine kuhojiwa muda mrefu.Kwamfano Eddy Mh.Riamy mwanamkakati wa ushindi, Mhe. Nassor Mazrui Naibu Katibu Mkuu, Mhe. Mahomoud Ally Mahinda Katibu Mtendaji JUVICUF Taifa, Mhe. Abeid Khamis Bakar, Mkuu wa Idara ya Habari na Uenezi JUVICUF. Jana pia Mkurugenzi wa Habari wa CUF taifa Mh.Hamad Masoud amekmatwa na kuwekwa kizuizini.

Zanzibar kuna kila aina ya manyanyaso na ukatili unaendelea kimya kimya na ni mateso ya hali ya juu kwa wananchi wasio na hatia.Kosa lao kubwa ni kutumia uhuru wao wakikatiba wa kukataa kufanya wasichokubaliana nacho.Haya yote yanaendelea kwa wananchi kwa shinikizo kubwa la CCM kufanya kila ukatili kuwalazimisha watu wakapige kura.

Jana Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Charles Kitwanga, alisema Zanzibar hakuna wanaopigwa ni hatari sana kwa kudanganya umma kwa kuficha ukweli na kuacha watanzania wateswe na kujifanya kiziwi kam vile wao si Watanzania. Kauli hii inaendelea kuwapa kiburi askari wake na mazombi kufanya unyama wanotaka Zanzibar.

CUF tunaendelea kutoa onyo kwa Serikali ya Magufuli watambue kwamba nchi hii ni ya wananchi na wanaweza kufanya watakalo muda wowote.

Ahsanteni

Magdalena Sakaya
NAIBU KATIBU MKUU

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.