Katika hali isiyo ya kawaida na baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu dhidi ya kile kinachokiita “njama za makusudi dhidi yake”, sasa Chama cha Wananchi (CUF) kinasema hakitaweza tena kuvumilia vitendo vya kihuni na kihalifu wanavyotendewa viongozi na wafuasi wake visiwani Zanzibar, kwani wameshasukumwa hadi kwenye ukuta.

Akizungumza na wakaazi wa Dunga Kiembeni, wilaya ya Kati Unguja, hivi leo (Februari 25), Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Mazrui, amesema hujuma ambazo zimepangwa na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuelekea kwenye kile kinachoitwa ‘uchaguzi mkuu wa marudio’, zinakusudia kuiingiza nchi kwenye machafuko. Akitaja mifano kadhaa ya vitendo hivyo vya hujuma, Mazrui alisema kitendo cha kuharibiwa kwa baraza ya CUF ya Dunga kilichofanywa usiku wa kuamkia leo kitakuwa cha mwisho kwao kukivumilia.

Kwa mengi zaidi, sikiliza hapo chini:

https://soundcloud.com/mohammed-k-ghassani/cuf-sasa-yachora-mstari

 

4 thoughts on “CUF yasema sasa imechoka na udhalilishaji”

  1. Tumshukuru Subhana na wale wote walohusika kushiriki kuachiwa kwa ndugu yetu Eddy Riyami na Inshallah mwenyenzi mungu amlinde na kila ubaya

  2. Mipango ya Seif Idi ni kwamba awakamate viongozi wa CUF na kuwapotezea maisha kama ilivyofanya ASP chini ya Karume enzi zile Zanzibar ilipovamiwa na Nyerere 1964

  3. Pengine wapo wale watakao sema kauli za Uchochezi Hali wakijua maneno ya naibu katibu wa chama ni kauli za Utetezi wa haki ya kila mmoja wetu kuheshimiwa na kulindwa ikiwa Tunahujumiwa ni Haki Kujitete.
    Hakuna njia ya Mkato hapo
    LINDA Na UHESHIMU Wazanzibari Wote

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.