“Kabla ya Serikali ya Kiingereza kuiingiza Zanzibar chini ya Himaya yake, Zanzibar ilikuwa ni Dola kamili iliyokuwa ina shughuli zake (ikiamiliana) na ulimwengu wote. Mara tu Muingereza alipoitia Zanzibar katika makucha yake mnamo mwaka 1890, kila jambo kubwa na dogo lilikuwa lazima liamuliwe kutokaUingereza. Mfalme wa nchi alifanywa kuwa ni alama tu ya Dola, hakuwa na uwezo katika kukata shauri juu ya uwendeshaji wa nchi. Kama ilivyo kawaida ya wakoloni popote ulimwenguni wanapotawala, lazima watumie mbinu za kuwagawa wananchi (ili waendeleze utawala wao) kutokana na hali za namna fulani ziliopo katika nchi. Ikiwa kwa njia za kidini, ukabila, urangi, utajiri, uwezo wa kimaisha na hata umadhehebu.” Soma kitabu cha “Ukweli ni Huu Kuusuta Uwongo” cha Aman Thani Fairooz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.