Salaams, kwanza nianze kwa kukusalimu. Pili, nichukue nafasi hii ili kuweka kumbukumbu sahihi kuwa maandishi yangu niliyoyaandika kuhusiana na kauli aliyoitoa Mh Zitto Kabwe ilikuwa na malengo ya kumfahamisha, na pia niliona umuhimu aliyoandika yalikuwa yanastahiki kupatiwa majibu kwa sababu yalikuwa yanapotosha jamii. Hili nitalielezea kwa undani na kwa lugha nyepesi ili tuelewane vizuri. Tatu, nachukua fursa hii kukushukuru Bw. Mohammed Ghassani kwa kudandia hoja na kuanika mawazo yako mazuri na kwa ustaarabu ili tuweze kujifunza au kwa lugha nyengine tuweze kufahamiana kwa undani kiasi fulani fikra zako, zangu na huyo Mh Zitto ukiwa mtetezi wake. Niseme, matarajio yangu, naamini ingekuwa ni vyema Mh Zitto Kabwe alistahiki kuja mbele yetu na kufafanua hayo mawazo yake aliyoyandika ambayo ni mafupi na hayana mbele wala nyuma. Nasema hivyo kwa sababu, Mh Zitto ni Mbunge na ana dhamana kubwa kwa wananchi wake pamoja na uwakilishi wake Bungeni katika kazi zake alizokabidhiwa na Watanzania.

Na Simai M. Said
Na Simai M. Said

Sasa, tuanze na utambulisho kidogo juu ya majibu uliyoyatoa Bw Ghassani. Binafsi, niseme nimepokea mawazo yako na nimeyasoma na nimefurahi kuona kuwa wapo watu wanaweza kujibu hoja hasa zinazo husiana na utalii. Umejitambulisha historia yako na imenisaidia wakati ninapoandika nijue uzoefu wako katika sekta mama ya utalii kwa hapa Zanzibar.

Kwanza, niseme, nilipomjibu Mh Zitto Kabwe, niliandika yale uliyoyasoma kwa kutumia uzoefu wangu na ninachokijua, na hapa tena ninaendelea kukujibu kwa kutumia uzoefu. Ila nitaweka mifano kwa ajili ya wengine wafahamu na kunielewa.

Sasa kwa kuanzia tuanze na Zanzibar wanakuja watalii wangapi na idadi yake hasa ni ipi. Nataka hapa unifahamu vizuri na ndo ndipo navunja na kuweka sawa majibu yako juu ya idadi ya wageni wanaofika. Tukubali kuwa hilo JIBU sahihi kulipata kwa Zanzibar ni GUMU na halipo. Kama unavyofahamu, sisi hapa Zanzibar tunaposema Watalii, tunakusudia WAZUNGU au watu wenye paspoti za nje. Sasa, kuna maeneo mawili makuu ya kuingia, Zanzibar ambayo ni Bandarini ( Seaport) na Uwanja wa ndege ( Airport ). Sasa SMZ wanachukua takwimu za wageni ambao wakitua ndani ya Uwanja wa ndege na pale wakiwa wanatoka safarini kutoka nje ya Tanzania na watatakiwa kujaza kadi za uhamiaji (arrival cards ) na zile ndizo hutumika kuwa zinatupatia idadi ya wageni waliotua hapa Zanzibar. Tumefahamiana hapo boss !! Sasa, wageni wanaotoka ndani ya Tanzania kama Arusha na Dar au hata mikoa mengine, wanapofika Uwanja wa ndege wanakuwa tayari wamo ndani ya Tanzania ( Domestic Arrival) sasa wale ni vigumu kuwajua idadi yao. Nakuachia wewe hapo kufanya na kusaka idadi yao. Hili nimelizungumza vikaoni mara nyingi na vikao vya juu kwamba inatuchanganya tunaposema wageni wamepungua au wameongezeka kwa sababu takwimu zetu haziowani. Sasa hilo ni eneo moja tunakosa idadi tunayohitaji. Eneo la pili, ambalo limetajwa na World Tourism Organization kuwa Mtalii ni nani ?

grafik
Hapa mnaweza mkaelewa yale nilioyasema juu idadi na takwimu. – Mwandishi wa makala

The World Tourism Organization defines tourism as people “traveling to and staying in places outside their usual environment for not more than one consecutive year for leisure, business and other.
Ina maana mtalii anaweza kuja kwetu kwa mapumziko au kwa biashara au mengineyo. Sasa kwa upande wa Zanzibar, sehemu tatu kuu TUNAZIKOSA au HATUZIHESABU kutokana na njia moja au nyengine. Sehemu ya kwanza ni wale wanaokuja kwa biashara na ya pili wanaofanya utalii wa ndani na ya tatu tunawaita JUNE JULY.
Tuanze na wa kwanza, hawa wanaofanya biashara, wanakuja kama na ndege au na boti na wanakuja kwa shughuli za biashara au mikutano. Wengi wao ni Watanzania wenzetu. Na wao wanahitaji malazi, usafiri na pia huishia kufanya matembezi. Hawa hawahesabiwi hapa Zanzibar kama ni Watalii.
Sehemu ya pili ni hawa tunawapokea sana kutoka bara kama kipindi cha Easter na Christmas au huja hata nyakati tofauti lakini wao huja na lengo la mapumziko. Sasa hawa kwa vile ni Watanzania wenzetu, basi hatuwahesabu na vigumu kujua idadi yao. Lakini hutumia wakati mwengine zaidi katika malazi na huduma nyengine kuliko hao wanaotoka Ulaya.
Sehemu ya tatu, ni hawa niliotoa mfano kama kwa umaarufu tunawaita June July. Hawa ni Wazanzibari wenzetu au wana udugu au wanakuja kuwatembelea ndugu zao hapa Zanzibar. Wao hukaa majumbani na muda wao unakuwa mrefu zaidi kwa sababu ya mahusiano na kwa lugha ya kitaalam wanaitwa “visiting friends and relatives”. Sasa hawa hutumia huduma tofauti kutokana na uwezo na mara nyingi huwacha fedha zao zote hapa Zanzibar kabla kurudi makwao.
Sasa, haya makundi matatu muhimu, huwezi kupata idadi yao pamoja nawale ambao niliowataja mapema ambao hufika Zanzibar kwa kutumia ndege za ndani.
Nilisema mwanzo, kuwa hoja yako ya idadi ya wageni haitakuwa kipimo kwa sababu takwimu ulizozitoa haziendani na hali halisi katika mwenendo mzima wa ujaji wageni hapa Zanzibar. SMZ kwa kupitia Kamisheni ya Utalii wanatoa idadi ya wageni kadri wao wanavyo amini lakini kwangu mimi hii idadi haina mashiko. Wanachotupa sisi hizi takwimu ni “indicators”. Wao wanahesabu direct arrivals unless kutoka mwaka huu wameamza kuwa capture hao wanaotoka mbugani. Hoja hii ninayo na niliizungumza sana nikiwa Mwenyekiti wa ZATI (2005-2010) na Mjumbe wa TCT ( Tourism Confederation of Tanzania) na pia kwenye Zanzibar Business Council mapema mwaka huu mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara Dr Ali M Shein.
Sasa kwa hapa, tumemalizana kwamba issue yako ya takwimu haipo na hutaweza kutumia kipimo isipokuwa kitakupa indicators. Pole sana, najua umehangaika kuzitafuta na mimi ninazo ila natumai sasa utakuwa umefunguka macho wazi na umepigwa mshangao. Ndo mambo kaka !!

Sasa tuje katika hizo hoja nilizozitaja kumjulisha Mh Zitto Kabwe ambazo wewe unapingana nazo au hujazielewa vizuri. Hizo hoja ambazo zipo sita kama ulivyozitaja na mimi niliziandika kwa kuzijua. Unajua, Bw Ghassani, kwenye tourism, kwa sasa kila jambo hukuzwa kutokana na ushindani wa biashara au kumlinda mtalii. Natumai uliona tukio la wasichana wale wawili waliomwagiwa tindi kali na jinsi lilivyopewa nafasi na vyombo vya habari vya ndani, nchi jirani na ulemwenguni.
Matukio ambayo nilioyazungumza juu juu kumelewesha Mh Zitto, yanaleta taswira isiokuwa na mvuto kwa mtalii. Sasa, matokeo kama haya, yanakuwa yanahitaji ufafanuzi mwingi kwa wageni huko nje na hasa yule ( Retail Travel Agents ) ambaye anauza hizo holidays kwa hao watalii. Sasa mgeni, anaweza akafanya booking yake miezi sita kabla, lakini viashiria vyenye sura isiokuwa ya kumvutia inaondoa ladha na hamu kwa mtalii kuja kwetu. Na ndio hizo sababu nilizozitaja zimechangia kwa kuzorota hii miaka ya karibuni. Sasa katika nchi ambayo una wavutia wageni waje kwa matembezi, ni lazima ujitahidi uwe na habari zenye mvuto zinapotoka nje. Sisi kama Tanzania, tumepata, lakini hatuwezi kuzifunika zile ambazo zimetuharibia. Kwa mfano, mazogo ya mjini ya Uamsho yaliotokea yaliandikwa na pia kufananishwa na mambo ya Islamic fundamentalism. Maoperators wengi ulaya walihoji kama waache kuleta wageni au wasimamishe kwa muda. Sasa matokeo kama hayo, huwafanya operators kutafuta destinations mbadala ila apunguze usalama wa mgeni na kujilinda yeye mwenyewe kama mfanyabiashara. Kwa hio, mimi kwa upande wangu, sihitaji wewe ukubaliane au ukatae ila nimejaribu kutoa ufafanuzi uelewe na wengine wafahamu kuwa kila jambo baya ndani ya nchi, hutuumiza kwa njia moja au nyengine kwa sababu kuwa tuna sekta tegemezi ya utalii na mzunguko wake wa shilingi ni mkubwa.

Kuhusiana na swala lako la kuwa mwaka jana wageni waliongezeka kwa 41%. Hicho kitu hakipo na haijawahi kutokezea. Kilicho ongezeka Zanzibar ni idadi ya wageni wanaokuja na kutua uwanja wa ndege wa Zanzibar ( Direct arrivals) . Na hili linatokana na kuongezeka kwa ndege ambazo zinatua Zanzibar moja kwa moja kwa mfano wakina Ethopian na wengineo. Kwa Zanzibar, pato kubwa lipo kwenye wageni wanaotoka mbugani ambao kwa mujibu wa aliyekuwa Mkurugenzi wa TTB Dr Nzuki ni 35% yao huja hapa. Hawa ni muhimu kwa sababu wapo huru na wanatumia huduma za magari na mengineo kila mmoja na lake. Na hapa ndipo tunapata lile kundi la wageni tunawaita kuku maana wao wanatumia zaidi kuliko hao wanaokuja na charters.
Kwa kuongezea, umetaja matokeo ya mwaka 2001 Januari na uzorotaji wa wageni ule mwaka. Ni sahihi kwa sababu, kwenye Feb/March/April ni kipindi cha hao travel agents kutayarisha hizo brochures za summer holidays kwa ajili mitandao na matangazo. Lakini pia huo mwaka kama ulisahau, tuliathirika hasa kutokana na tokeo kubwa New York la 9/11. Tukio lile liliathiri usafiri kwa ujumla duniani kote na hata sisi kwenye ujaji wa wageni hata mwaka 2002. Na huo ndio mwaka ambao ZATI ilizaliwa ili kukabiliana na changamoto za sekta ya utalii za ndani na nje kwa niaba ya sekta binafsi.

Kwa kumalizia, sijaona eneo ambalo umeweza kuonesha kuwa hoja zangu nilizozitaja kuwa hazina mashiko. Zipo wazi na vitendo ambavyo vilitokea bado vinatuandama. Tunachohitaji kuwa tunapeleka salamu pamoja habari zenye mvuto kwa wageni na marafiki ili wageni wajiskie kuja kwa matembezi kwetu.

Swala la kufutwa kwa uchaguzi ni jambo la mpito na sio kipimo hata kidogo kwa kuzorota ujaji wa wageni miaka ya karibuni. Kama litakuwa ni issue basi ni la kwetu sisi ndani ya nchi na inawezekana wageni wengi hivi sasa wala hawajui na kuelewa hayo maswala ya uchaguzi. Na hilo linaendana na mfumko wa bei lilitokana hivi karibuni kutokana na supply na demand. Nilipokuwa Mwenyekiti wa ZATI tulifanya study ya value chain analysis juu ya mboga mboga, na tuligundua kuwa mboga mboga nyengine hupitia mikononi au kwa madalali mpaka saba kabla kufika mezani kuliwa. Sasa hapo unaweza kufikiria jinsi mfanya biashara anavyojiongezea faida au kujivutia upande wake. Kinachohitajika hapa ili kupunguza makali kwa wananchi ni kuangalia kwa undani swala la food inflation kwa kuweka mipango maalum baina ya serikali kwa kushirikiana na kama Chamber of Commerce ya Zanzibar ili kuweza kukabiliana na hayo mahitaji ya wananchi.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.