Ikiwa zimebakia wiki tatu kufanyika uchaguzi mkuu nchini Tanzania, wasiwasi unaongezeka kuelekea kile kinachoangaliwa kama uchaguzi wenye ushindani mkali zaidi kwenye historia ya nchi hiyo, huku kwa mara ya kwanza chama tawala, CCM, kikikabiliwa na uwezekano wa kushindwa kwenye uchaguzi tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.

Mgombea wake wa urais wa Jamhuri ya Muungano, John Magufuli, amejikuta na kibarua kigumu sana katika jitihada zake za kumrithi Rais Jakaya Kikwete ambaye anaondoka madarakani baada ya kumaliza mihula yake yake miwili anayoruhusika kikatiba.

Magufuli, mwenye umri wa miaka 55, anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mgombea wa upinzani, Edward Lowassa, ambaye anasimama kwa niaba ya vyama vinne vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA). Lowassa, mwenye umri wa miaka 62, alikiacha chama chake cha zamani, CCM, na kujiunga na chama kikuu cha upinzani, CHADEMA, kuongoza muungano huo wa vyama mwezi Julai. Endelea…

 

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.