Ningalia

Published on :

Lau nabagwa machozi, Zenji nikakulilia Si kwamba mimi bazazi, au ni mwana mviya Bali ni yangu mapenzi, kwako yalonizidia

Mneni Mnena Mno

Published on :

Mnena mneni mno, haneni jambo aula Huwa anena maneno, ya kuuvunja muwala Ya kuzuwa mivutano, na mashaka na madhila Ikabaki lahaula, pasiwe na mapatano