Kabla ya kuja kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kulitanguliwa na nchi mbili zilizokuwa na uhuru na mamlaka kamili, Tanganyika na Zanzibar. Tanganyika ilipata uhuru wake tarehe 9 Disemba 1961 unaohusishwa sana na mchango mkubwa wa chama cha TANU na uongozi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Panaweza pakawa na mjadala juu ya ukubwa wa mchango huo lakini hakuna mjadala kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa kinara wa kupigania uhuru kwa taifa hilo la Tanganyika, taifa ambalo jina na utaifa wake vilipotea kiajabu kwa kile kilichokuja kuitwa “Muungano wa Tanzania”.

Kwa upande wa Zanzibar ingawa historia zinakingana kutokana na mazingira na matukio ya wakati huo, lakini kwa hapa nataka niungane na wale wanaomini kwamba ilijipatia uhuru wake tarehe 12.01.1964, ambapo yalifanyika mapinduzi ili kupatikana uhuru wa nchi hiyo, ambapo mapinduzi hayo yalisimamiwa chama cha A.S.P chini ya kiongozi wake Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.

Na Ali Mohamed
Na Ali Mohamed

Katika mwaka huo huo wa uhuru wa Zanzibar kupitia mapinduzi, Mkataba wa Muungano ulitiwa saini na Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964, Zanzibar. Ulithibitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi Aprili 26, 1964, na Aprili 27, 1964 viongozi hao walikutana katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Dalaam kubadilishana hati za Muungano.

Sheria za Muungano ilitamka kwamba, Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zililazimika, kuwa dola ya Jamhuri kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, jina ambalo lilibadilishwa Oktoba 28, 1964 na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia sheria ya Jamhuri ya Muungano, sheria namba 61, ya mwaka 1964. Msingi wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ni Hati za Muungano za Mwaka 1964.Hati za Muungano zilitiwa saini na Nyerere na Karume, Aprili 22, 1964 na hapo Tanganyika na Zanzibar kuwa dola moja kwa misngi inayotambulika kimataifa. Baada ya kuungana, Mwalimu Nyerere alikuwa rais wa kwanza na Karume alikuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aprili 26, 1964, bunge la Tanganyika lilipitisha sheria za Muungano, ambazo baadayezilithibitishwa na Baraza la Mapinduzi Zanzibar. Mnamo Aprili 27, 1964 waasisi wa Muungano walibadilishana Hati za Muungano na wajumbe saba wa Baraza la Mapinduzi waliapishwa kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Watanganyika na Zanzibar ambao ni Amani Karume, Kassim Abdallah Hanga, Abdulrahman Babu, Hassan Nassor Moyo, Aboud Jumbe, Hasnu Makame na Idris Abdul Wakil. Kati yao, Aboud Jumbe na Hassan Nassor Moyo wangali hai.

Utangulizi wangu mrefu wa hapo awali ni kutaka kuonyesha usawa uliokuwepo wakati wa muundo huo wa muungano wakati wa uundwaji wake hadi kusimama kwake, ambapo ulipofika wakati wa utekelezaji wake muungano huo ndipo ukaanza kupoteza usawa kiasi ambacho ule upande uliohisi hautendewi haki ama unapunjwa ukaanza kulalamika tangu miaka ya mwanzoni hadi kufikia sasa.

Ningependa niseme kwamba hatuwa na juhudi mbali mbali zinafanywa kuuendeleza muungano huu mda mwengine hata nguvu za ziada hutumika ili kuuwezesha muungano huu uendelee kudumu ambapo kwa juhudi hizo umeufanya utimize miaka 51 ya kuepo kwake.

Wapo wanosema kwamba iwapo utakuwa katika muundo tofauti na ulivyo sasa basi wangependa uwepo hadi milele, hali kadhalika wapo wanaosema wanataka udumu kwa mfumo huu huu uliopo, kwa hawa wanaoamini mfumo huu uendelee kama ulivyo ni kwa kuwa tu hiyo ilikuwa nia njema ya waasisi wake ambao ni vipenzi vyetu sote watu wa pande hizi mbili, lakini huku wakisahau kwamba walipokubaliana kuungana walikubaliana kuwa na haki sawa kwa kila upande.

Waasisi wetu hawa wote wameshatangulia mbele ya haki wote, sasa tunapofikia hatuwa ya kuwasifu kwa lengo la kudumisha muungano kwa nini tumtumie muasisi wa upande mmoja tu ili kurekebisha ama kuelezea masuala yanayohusiana na muungano?

Nimewahi kusikia mara nyingi hasa kupitia chama tawala CCM bara na visiwani, iwe katika mikutano ya hadhara, Mikutano ya vikao vya Bunge/Baraza la Wawakilishi, mikutano na waandishi wa habari na kadhalika, akitanjwa na kupewa sifa pekee Marehemu Julius Kambarage Nyerere juu ya muungano, iwe sifa hizo ni kwa ajili ya kuonyesha marekebisho ya kero zilizopo za muungano, iwe kwa kujaribu kuulinda ili uendelee kuwa katika mfumo uliopo, iwe kuonyesha umuhimu wake.

Marehemu karume ni mshiriki halali na muasisi wa muungano, yeye pia nina uhakika ameuzungumzia sana muungano huu na amekuwa akifanya juhudi kuulinda kwa njia zake anazoziamini zitaudumisha kwa dahari nyingi, kinachoniuma na kunishangaza, kwa nini isiaminike kwamba njia zake na yeye zitumike kuulinda? Kwa nini njia za Kuulinda muungano za Mwalimu Nyerere pekee ziwe ndio njia sahihi? Jee hakuwahi Mzee Karume Kuzungumzia muungano wakati wa uhai wake? Jee hakuwahi kutoa rai za kujenga muungano bora ambao utaondoa yale matatizo yaliyoitwa na Mwalimu Nyerere kuwa si matatizo bali ni kero zinazotatuka?

Kwa nini basi iwe sifa nyingi za Mwalimu J. K. Nyerere zitumike kama falsafa ya kudumisha Muungano na kuzidogosha za Marehemu Abeid Amani Karume? ambapo yeye kama alivyokuwa Nyerere ni muasisi wa Muungano wa Tanzania na yeye Karume ana sifa sawa na haki sawa katika muungano huo.

 

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.