Kuna baadhi ya kesi ambazo serikali huziwasilisha mahakamani kwa jina la “Jamhuri”, huhitaji kwanza ishinde kesi hizo kwenye jamii, miongoni mwa wananchi. Hizo ni zile zinazowahusisha viongozi wakubwa wa ama vyama vya kisiasa au taasisi za kijamii ambao kwa kupingana kwao na serikali iliyopo madarakani, serikali hiyo huamua kuwatia adabu kwa kutumia mfumo wa kawaida wa kimahakama ili ionekane kwamba ni sheria iliyokuwa imechukuwa mkondo wake na sio kwamba ni siasa iliyoingilia kati mkondo wa kisheria.

Viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu wakiongoza wananchi kwenye maandamano ya kutaka mamlaka ya Zanzibar yaheshimiwe.
Viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu wakiongoza wananchi kwenye maandamano ya kutaka mamlaka ya Zanzibar yaheshimiwe.

Kwetu kadhia hiyo ni pamoja na kile kilichopewa jina la kesi ya ugaidi inayowakabili viongozi na wafuasi 28 wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu ya Zanzibar, maarufu kama Uamsho, ambayo sasa inakata mwaka wake wa pili ikiwa haijafika hata hatua ya kuitwa kesi kamili kwenye mahakama za Tanzania Bara, lakini tayari makubwa na mabaya yakiripotiwa kuwapata viongozi hao. Kwenye kadhia hii, serikali zote mbili, ya Muungano na ya Zanzibar, zilishindwa tangu awali kwenye hisabati zao za kisiasa. Hazikushinda kesi hii machoni pa umma na ndiyo maana hadi sasa upande wa mashitaka, ambayo ndizo hizo serikali zenyewe, umewawia vigumu kushinda mahakamani kwenyewe.

Wafuasi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) upande wa Zanzibar pamoja na viongozi wao hawafichi chochote kuhusiana na kesi zinazowakabili viongozi hao wa Uamsho. Amesikikana Waziri Haji Omari Kheri, Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi na makada kadhaa wa chama hicho wakisema waziwazi kwamba kinachowapata Uamsho kina mkono wao, na wenyewe huyasema hayo kwa kujisifu kuwa ni kigezo cha kuwatisha wengine wowote ambao wanaonesha kupingana na siasa za CCM visiwani humo.

Lakini hapa kwenye Zanzibar Daima bado tunafungwa na kanuni za uandishi kuzungumzia kesi iliyoko mahakamani kwa kile kinachosemwa kisheria kuwa mazungumzo yetu yanaweza kuingilia uhuru wa mahakama na kuathiri mwenendo wa kesi husika. Hata hivyo, hapa tunaweka tu mjadala wa siku ya Alhamisi ya tarehe 21 Mei 2015 bungeni, ambapo suala la madhila yanayowapata viongozi wa Uamsho ulirindima kwa nguvu kubwa bungeni.

Hukumu ni yako mwenyewe msomaji.

2 thoughts on “Serikali imeshindwa na Uamsho kisiasa, haitawaweza mahakamani”

  1. Hao viongozi wanaojigamba kuwa wanehucka kuwahujumu mashekhe wetu wajue kwamba walikuwepo wenye nguvu zaid yao na madaraka na mungu amewakamata kwa nguvu na kuwaangamiza ni wajibu wao wasome hictoria ya majeur kama wao waliopita yepi yaliwashukia kishaa ndo wafanye hizo dhulma zao na mungu ameahid kumnusuru aliyedhulumiwa hata kama kwa muda wa baadae naa atamuangamiza dhaalimu allah awatue mashekhe wetu ktk makucha ya mafusad inshaallaah

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.