Viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu walitimiza wajibu wao kwa nchi yao ya Zanzibar. Kilichowapata na kinachowapata kwa kutekeleza wajibu huo tunakishuhudia kwa macho na tunakisikia kwa masikio. Kesi yao iko mahakamani sasa wakituhumiwa kwa ugaidi. Kanuni zinatufanya tusizungumzie mwenendo wa kesi, eti kwa kuwa kuzungumzia kwetu kunaweza kuathiri kesi yenyewe.

faridi
Sheikh Farid Hadi

Hata hivyo, viongozi waliowahi kuwa na ufuasi mkubwa kwenye mikusanyiko ya hadhara ndani ya visiwa vya Zanzibar, sasa wanaumizwa na ukimya wa Wazanzibari wale wale waliowaamini wako pamoja nao.

Lakini kama sisi tumeamua kukaa kimya kutokuwasemea, wenyewe hawajanyamaza. Bado wanasema. Na wanasema kile kile – hali ya Zanzibar ndani na nje ya Muungano. Msikize hapa Sheikh Farid Hadi akiwa mahakamani wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.