Niende moja kwa moja kwenye nukta yangu. Mwaka huu wa 2015 tunaouita kuwa mwaka wa maamuzi unamaanisha kwamba, ndiyo, tutajiandikisha kwa wingi kuwa wapiga kura na kisha, ndiyo, tarehe 25 Oktoba tutashuka kwa wingi vituoni kupiga kura hizo. Lakini usichomaanisha ni kuwa tutarudi nyumbani kupika wali kusubiri matokeo yatangazwe. Hapana. Tutailinda kura yetu.

zecNa tunapouchukulia uchaguzi kama mchakato wenye matendo na matukio mengi ndani yake, tutajuwa kuwa ulinzi wenyewe hasa lazima uanze sasa na wala si kesho. Kumbuka kwamba si jeshi la polisi, si serikali hii iliyojaa hujuma, si Tume za Uchaguzi, si UNDP, wala si mwengine yeyote, bali ni sisi wenyewe. Tukiwa ni wazalendo tunaoumwa na nchi yetu, hatuna budi kulinda kura zetu ili tupate haki yetu ambayo ni ushindi utakaotupatia nchi yetu.

Na Ali Mohammed Ali
Na Ali Mohammed Ali

Ninaposema tuanze kulinda kura na ushindi wetu kuanzia sasa, ninamaanisha nini? Ukiwa wewe ni sehemu ya jamii hii iliyonyimwa haki tangu ulipofumbua macho yako kuuona ulimwengu, unatakiwa kuanzia sasa ufanye ushawishi katika kikundi kinachokuzunguka. Waelimishe wenzako umuhimu wa nchi kubakia mikononi mwa Wazanzibari kwa kadiri ya uwezo aliokujaalia Mungu.

Wape mifano hai iliyopo. Kwa mfano, waambie ni furaha iliyoje kuona rais wetu ameweza kugawa mikoa bila ya kupata ridhaa kutoka Bara, lakini pindipo wakipoteza kura kwa kuipigia CCM, watakuwa wameitoa muhanga Zanzibar yetu, maana hicho ni chama ambacho kimeahidi kuipoteza Zanzibar kwa kauli yake kupitia kwa viongozi wake.

Siku wakiwapa kura na kuinuka na ushindi, maana yake ile katiba inayolalamikiwa kila kona kwamba itaipoteza Zanzibar ndio inafanya kazi. Hivyo rais wetu hatoweza tena kugawa mikoa kirahisi kama alivyofanya juzi kwa dakika tano tu, kwani kwa mujibu wa katiba hiyo atatakiwa apate ruhusa kutoka Bara.

Waambie j,e hawaoni fahari kuchagua rais wanayempenda wenyewe hapa hapa Zanzibar na kuachana na kuchaguliwa watu wasioridhika nao ambao hutoka Dodoma, ambao wakipewa madaraka basi huwa hawana budi kulipa fadhila za Dodoma na sio kuwalipa fadhila Wazanzibari?

Waambie kwamba hivi sasa kila siku tunagombana sisi wenyewe kuhusiana na umiliki wa ardhi. Wakipoteza kura zao kwa kuipigia CCM nayo ikaihalalisha katiba hiyo, basi wajuwe wameumia wenyewe, kwani Kifungu cha 23 (a) cha Katiba hiyo kinawapa uhalali Watanzania wote, hata wasiokuwa Wazanzibari, kumiliki ardhi yetu iliyo ndogo.

Wakumbushe ndugu zako hao kwamba iwapo watadharau haya, wakumbuke kwamba tumekuwa na ugomvi wa hali ya juu na Tanganyika kwa miaka mingi juu ya uchimbaji wa mafuta yetu machache ambayo Mungu hakukosea kututengea sisi kutokana na udogo wetu. Basi akumbuke endapo ataipigia kura CCM na kupata ushundi kwa kura yake, hivyo ndivyo kutoa ruhusa mafuta hayo yachimbwe na Watanganyika kwani ibara ya 26 ya katiba mpya ambayo itatumiwa baada ya uchaguzi inaeleza waziwazi kwamba mafuta na maliasili zote ni mali za umma na Serikali ya Muungano au serikali ya Zanzibar itasimamia uchimbaji wa mafuta. Hivyo hapa Serikali ya Muungano haitosubiri Zanzibar waamuwe kwa kuwa Serikali ya Muungano ndiyo iliyopewa haki mwanzo na katiba hii.

Wameshatangaza kupitia kipindi cha televisheni. Tulimsikia mbunge wa Magomeni kwa tiketi ya CCM akitamka bayana kwamba yeye ni muumini wa serikali moja, akimaanisha Serikali ya Zanzibar isiwepo na hapo kiusahihi wake ni kwamba Zanzibar itabakia kuwa sehemu ya Tanganyika iliyojipa jina la Tanzania, yaani Zanzibar itakuwa moja ya mikoa ya Tanzania tu.

Pia waambie athari za kudhulumu na madhara yake kwa kupiga kura zaidi ya moja kuipigia CCM kwa kurubuniwa na shilingi 10,000/= hata milioni 10,000,000/=, ili tu kuifanya CCM ishinde, basi waambie kwamba hilo ni deni la raia wote na hatoweza kulilipa.

Kumbuka wewe ni mlinzi wa Zanzibar yako uipendayo, ambayo utaulizwa kwayo ni namna gani ulitumia uhai wako kuilinda.

 

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.