Idhaa ya Kiswahili ya Deustche Welle nchini Ujerumani imeanzisha kampeni maalum ya mwezi mmoja (Machi 2015) kuongeza nguvu kwenye mapambo dhidi ya ukatili wanaotendewa watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Tanzania.

Kwenye mfululizo wake wa makala, ripoti na mahojiano na watu mbalimbali, asasi za kijamii na mashirika ya kimataifa ndani ya Tanzania na maeneo mengine ya Afrika Mashariki, DW inakusudia kuyaelezea maisha na jaala za watu wenye ulemavu wa ngozi nchini humo.

Katika wakati ambapo msimu wa uchaguzi umewadia, vitendo vya kuwashambulia, kuwauwa na kuwakata viungo vyao watu hao wenye ulemavu wa ngozi (albino) vimeanza kujitokeza tena na kushika kasi.

Inaaminika kuwa mauaji hayo hufanyika kwa imani za kishirikina zinazochochewa na masuala ya kisiasa na kibiashara.

Kufuatilia na kuwa mshiriki wa moja kwa moja wa kampeni hii ya mwezi mmoja, bonyeza hapa.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.