Nimewahi kusema kuwa kuna haja ya kutumika busara ili Kura ya Maoni isifanyike kabisa mwaka huu na niliungana na wale waliokuwa na fikra kama hiyo, hadi pale wenzangu walipobadilika.

Walibadilika kwa sababu walikuwa na lengo la kisiasa. Walichukulia fursa ya kufanyika Kura ya Maoni na ushindi utaopatikana kama ikipita ni sawa na kukifyagilia njia Chama cha Mapinduzi kwa ushindi wa Uchaguzi Mkuu kote Bara na Zanzibar.

Na Ally Saleh
Na Ally Saleh

Hoja yangu wakati huo ilikuwa ni kuwa Kura ya Maoni kwa hadhi zote ni sawa na Uchaguzi Mkuu maana huwa na kipindi cha elimu ya mpiga kura, kisha huwepo na kampeni na kuwepo pande zinazopingana katika hicho kinachopigiwa kura na kwa hili la katiba, ni dhahiri kutakuwa na kazi kubwa.

Kazi kubwa maana yake pande zinazotaka katiba ipite na isipite zote zimeshanowa visu kwa ushindani mkali na bila ya shaka kutapelekea kuwepo mvutano, uhasama nap engine hata magomvi ambayo huambatana na uchaguzi katika mazingira yetu ya Kiarfika zaidi.

Wasiwasi wangu ni kuwa kunaweza kukawa na chaguzi nne katika nchi kwa mwaka mmoja kwa maana ya Kura ya Maoni ya April 30 na iwapo itarudiwa kwa kupigwa HAPANA mara ya kwanza.

Kisha kufuatiwa na Kura ya Maoni ya Wazanzibari kupitisha hiyo Katiba Pendekezwa na mabadiliko yake kwa Katiba ya Zanzibar ya 1984 na kisha Uchaguzi Mkuu wa 2015 mwezi Oktoba.

Aliyekuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Alley Said.
Aliyekuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Alley Said.

Naionena huruma sana Zanzibar yangu ambayo itakuwa na chaguzi zote hizo wakati tunajua mara nyingi chaguzi huirarua Zanzibar vipande vipande na tumeanza kupata afueni hivi karibuni tu kwa kuundwa Serikali ya Pamoja baada ya mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ya 2010.

Na hali imeshaanza kujitokeza kutaka kuvunja Serikali ya Umoja wa Kitaifa kiasi ambacho inawezekana kabisa wakati tukifanya mabadiliko ya Katiba Pendekezwa kwa mnasaba wa Katiba ya Zanzibar kukawa na shindikizo pia la kuvibadilisha vifungu vya Serikali ya Umoja wa Kitafia jambo ambalo wahafidhina ndani ya CCM wamekuwa wakilisema jahara.

Uwepo wa Kura ya Maoni ni jambo la kisheria  na kwa kweli ni hatua ya lazima kupata Katiba Mpya.  Lakini si jambo la kufa na kupona kwamba lazima lifanywe kwa tarehe maalum au muda lazima uwe sasa na ndio maana Rais Kikwete alikuwa amekubaliana na vyama vya siasa vilivyo chini ya mwamvuli wa Tanzania Democracy Council (TCD).

Muhammad Yussuf Mshamba, aliyekuwa mjumbe wa Kamati ya Katiba.
Muhammad Yussuf Mshamba, aliyekuwa mjumbe wa Kamati ya Katiba.

Na kwa kweli hicho ndicho ambacho sasa kimejitokeza kwamba nchi, yaani taasisi husika na Serikali yenyewe hazijakuwa tayari kwa Kura ya Maoni.

Kama leo ni Februari tayari hakuna muda wa kutosha wa maandalizi kuanzia ya uandikishaji wapiga kura kwa njiaya eltroniki yaaani BVR lakini pia mipango mengine inayoambatana na kura hiyo. Muda huu ulikuwa ndio muafaka wa kuwa na suali la kuulizwa kwenye kura hiyo, makundi yanayotaka kuwa wapiga kampeni ya HAPANA na NDIO yawe tayari yanaelekea kujiandikisha na pia tuone harakati za elimu ya wapiga kura zikianza kuwekwa bayana na Tume ya Uchaguzi.

Hakuna lolote linalofanyika la kuutia umma imani kuwa kweli kuna mambo yanayotoka au pengine ni kwa sababu ya usiri? Jee umma unaweza kuwekwa nje ya kujua jambo hili kwa kiasi chote hiki?

Kwa sababu hizo basi ndio kukaanza kuzuka kundi jengine kabisa, na khasa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA ambao umekuja na mpya kuwa wao wanasusia kabisa mchakato kupita Kura ya Maoni kwa sasa sababu kuwa hakitapatikana kilichokusudiwa.

Ibrahim Hussein, mwandishi na mwanaharakati wa Zanzibar.
Ibrahim Hussein, mwandishi na mwanaharakati wa Zanzibar.

Wao wanaona, hasa kwa vile waliukimbia mchakato huo katika Bunge Maalum la Katiba, kuwa hapana liwalo na Kura ya Maoni haina tija kwa aina ya katiba inayopelekwa kwa wananchi yaani ile inayoitwa Katiba Pendekezwa ambayo ni shikilia la Rais Kikwete na Chama cha Mapinduzi.

Pili, wanaona ni haramu kitu ambacho walikikataa katika utengejezaji wake kisha warudi wakipigie kura kukihalalisha. Wanasema hiyo abadan na tayari wamewataka wanachama wao na wanachi wasusie kura hiyo. Taasisi nyengine pia kama Kituo cha Haki za Binadamu (HRLC) wametoka wazi wazi wakisema katika hiyo haifai kupigiwa kura ya kuungwa mkono ingawa wao wanataka wananchi wakapige kura na waikatae Katiba Pendekezwa.

Mimi kama Mzanzibari nataka nijihusishe zaidi na ubaya wa Sheria ya Kura ya Maoni ambayo ndio inayoongoza taratibu nzima za kura hiyo na ambayo ina madhara makubwa kwa Zanzibar.

Omar Mussa Makame, mmoja wa wachangiaji wa mdahalo wa Katiba Mpya.
Omar Mussa Makame, mmoja wa wachangiaji wa mdahalo wa Katiba Mpya.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 34 cha Sheria hiyo kura za upande wa Zanzbar, ambapo kila upande ili kura zipige itahesabiwa kwa zaidi ya asilimia hamsini, zinaweza kuwana mashakil makubwa. Sheria hiyo inasema kura za Zanzibar zitatoka sehemu tatu.

Kwanza wapiga kura wlaiondikishwa na ZEC yaani Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar, na hilo halina mashaka na orodha yake tunaijua, japo ina mivutanovutano.

Pilii wapiga kura pia watakuwa ni watu walioandikishwa na Tume ya Uchaguzi ya Tanzania NEC ambao wanaishi Zanzibar na hapa wengi tutajiuliza juu ya uhalali wa Watanzania hawa kupiga kura kwa kapu la Zanzibar na kama Wapemba wanavyosema vyereje?

Lakini kali zaidi ni kifungu hicho kusema kuwa kura za kapu la Zanzibar pia zitahesabiwa kwa Wazanzibari ambao wanaoshi Tanzania Bara na ambao wameandikiswa kwenye daftari la NEC.

Hapa mtu unajiuliza ilikuwaje mpaka yafike yote haya wakati hivi sasa Wazanzibari hao hao wananyimwa fursa ya kupiga kura kwao na hata wale walioko kwao wanakataliwa kwa sababu ya ukaazi?

Bi Hassanati, mchangiaji wa mdahalo wa Katiba Mpya.
Bi Hassanati, mchangiaji wa mdahalo wa Katiba Mpya.

Basi katika sakata lote la Kura ya Maoni hili ndilo ambalo mimi linaniuma zaidi. Ya nini hadaa na janja yote hii ya kuwanyima Wazanzibari sauti yao ya kuamua?

Hivi ndio maana wakubwa wakawa na hakika kuwa kura itapita tu vyovyote iwavyo? Na kwa kweli itapita kama sheria imeelekeza kama hivyo.

Na kwa sababu hiyo naungana na wale wote wanaosema kuwa njia mbadala ni kususia kura hiyo na kama ikipita dunia ijue kuwa sauti ya umma imesokotwa na maamuzi ya kura hiyo ni ya hadaa na kijanja.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.