Leo ilikuwa ni siku adhimu sana kwa Wazanzibari siku ambayo ilitangazwa elimu bila malipo kila ifikapo siku kama hiyi wanafunzi huisherekea kwa kwaya ,michezo ya kuigiza ,mbio za vijiti aina mbali mbali za mipira na mashairi kwa hakika wanafunzi mbali mbali hupokea zawadi kwa ushindi kulingana na michenzo waliyoshiriki na baada yake zawadi ya wanafunzi bora hutolewa .

Mara nyingi sherehe hizi hutanguliwa na maandano ya skuli mbali mbali na mwisho mgeni rasmi huadhimisha kwa kuwahutubia wanafunzi ili kufikia kilele cha sherehe hizo ambazo huadhimishwa kila mwaka hapo zamani tulikuwa tukifurahia sana sherehe hizo kwani ilikuwa ni fursa mmoja ya kuweza kusafiri kutoka Pemba kuja Unguja au kutoka Unguja kwenda Pemba.

Kwa kadri miaka inayoendelea ndio sherehe hizi zinavyokumbwa na misukosuko huku kukiwa tayari ile dhana mzima ya sherehe za elimu bila malipo haipo tena , na kiwango cha elimu kimeshuka huku Zanzibar ikiendekeza siasa na kuacha mambo yenye maana kwa hatima ya taifa lao waliokuwa hawakusoma bado wananguvu na kulipeleka taifa mrama kwani dhana ya kuwa aliyekwenda skuli achukue nafasi yake haipo kubwa ni kuwa mzee wako mkereketwa inatosha kuchukua ulua.

Ninapohamu mimi wizara ya elimu ni chombo ambacho bajeti yake si ya muungano lakini kimekumbwa na wimbi kubwa la wafanyakazi wa mahotelini ambao huhamia Zanzibar na watoto wao na kuwanyima fursa Watumbatu ,Wamatemwe ,Wapaje na Wakizimkazi kwani wao fursha yao ni hapa nyumba wakipata wakikosa angalau wezetu wanaweza kurudi nyumbani na wakapata fursa hiyo.

Hebu angalia ikiwa kuna wafanyakazi elfu 6000 wa mahotelini ambao wametoka nje ya Zanzibar na wakaja na mtoto mmoja kweli wizara ya elimu inaweza kuhimili hili ?ukiachilia mbali milango iko wazi kwa Wakenya,Wakongo na Wanyaruwanda mtoto wa darasa la kumi na mbili la Zanzibar ataweza kuchuana nao ?si hili baada ya sisi kufa watakuja wawafanye watumishi wa maofisini watoto wetu ?hili nalo linaonyesha siku mmoja itakuwa kweli ndio maana skuli zetu zimefurika watoto .

Shibe iwapi katika skuli zilizokuwa zinalaza wanafunzi huku mabuku na seti za hisabati zenye daraja la kichina zikiwa zimeshatoweka katika macho yetu maskini iwapi sherehe hapo ?kama kuna mtu ambae anafaa kupongezwa ni yule aliyetengeneza fomula hii ya kuwakosesha elimu Wazanzibari amepasi sana nampongeza kwani suala zima la janja weed lisingalikuwepo kwani sifikirii kama wao wamesoma wale wasingalihangaishwa na baada kutumiwa wakaachwa solemba.

Tayari kambi zimeanza kidogo kidogo huku wengine wakiishia kunawa tuu baada ya uchanguzi na kushindwa pakushika nidhamu maskulini haiku tena zaidi ya mwanafunzi kuweza kumkabili mwalimu wake na kumwambia maalimu nakupenda ,mapenzi matupu baada ya elimu kitu ambacho kwetu ilikuwa ndoto eti maalimu amtie mimba mwanafunzi wake duu ?kuna minongono kuwa bara wanataka kubadilisha mfumo wa elimu.

Jamani tuacheni masihara au dhihaka elimu ndio ufunguo wa maisha au sababu watoto wetu nyie mawaziri munapelekea skuli za kulipia kwa hiyo haiwahusu hili la baka wa biti hatibu haya bwana jitengezeeni mazingira ya tabala la watawala na wataliwa huku uhuni miongoni mwa wanafunzi wetu ikiwa ndio sehemu kubwa mambo wanayojifundisha ndungu zetu leo,wengi wao hawajielewi na ndio maana hukata tamaa mapema na kujiingiza katika janga la utumiaji wa madawa ya kulevya.

Makala na picha na Mwandishi Wetu