Mwenyekiti wa Jumuiya ya Zaka na Sadaka Zanzibar (JUZASA) Shekh Said Suleiman Masoud akizungumza katika mkutano wa Jumuiya hiyo uliofanyika Ukumbi wa Shamtimba Kiembesamaki Zanzibar.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Zaka na Sadaka Zanzibar (JUZASA) Shekh Said Suleiman Masoud akizungumza katika mkutano wa Jumuiya hiyo uliofanyika Ukumbi wa Shamtimba Kiembesamaki Zanzibar.

Kukosekana kwa Utaratibu nzuri wa Utoaji na Usambazaji wa Zaka ni moja ya matatizo yanayopelekea Zanzibar kuendelea kuwa na Watu wanaoishi katika mazingira magumu na Umasikini uliopindukia.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Zaka na Sadaka Zanzibar (JUZASA) Shekh Said Suleiman Masoud ameyasema hayo alipokuwa akitoa nasaha katika Mkutano wa Jumuiya hiyo uliofanyika Ukumbi wa Shamtimba Kiembesamaki Zanzibar.

Amesema Zanzibar kuna watu Wenye nafasi nzuri kiuchumi lakini  wanashindwa kutoa Zaka katika utaratibu Unaofaa na hivyo kushindwa kuwafikia Walengwa wenye Mahitaji.

Amesema Watu hao wenye uwezo wangekuwa wanatoa Zaka na kusambazwa katika utaratibu unaofaa, Zanzibar ingekuwa haina Watu Masikini kutokana na Zaka hizo kuwakomboa katika kiuchumi.

Sheikh Said amesema wameamua kuanzisha Jumuiya ya (JUZASA) ili kurahisisha Upatikanaji na Usambazaji wa Zaka baada ya kukosekana jambo hili kwa miaka mingi.

Ameongeza kuwa kwa muda mrefu Zanzibar kumeundwa Taasisi nyingi za Serikali na za kibinafsi kwa ajili ya kumkomboa Mwananchi na Umasikini lakini malengo yanashindwa kutimia kutokana na kukosekana Elimu ya Utoaji wa Zaka.

Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya ya JUZASA Omar Abubakar ameelezea Malengo ya Zaka kuwa ni pamoja na Kuitakasa Mali ya Mtoaji na kumkomboa Muislamu kutokana na Janga la Njaa.

Ametoa wito kwa Waislamu kujitokeza kuwaunga Mkono sambamba na kupeleka Zaka zao katika Jumuiya yao ili Waziwasilishe kwa walengwa wanaofaa kupewa Zaka katika jamii.

Katika Mkutano huo Jumuiya hiyo imefanya Uchaguzi ambapo Mwenyekiti wake na Katibu wake wamechaguliwa tena kuiongoza Jumuiya hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu.

Jumuiya hiyo iliyopata Usajili mwaka 2011 inapokea na kusambaza Zaka kwa walengwa,ambapo malengo yake makuu ni kutekeleza vyema Suala la Zaka ili kuweza kuwasaidia Wanajimii wanaoishi katika mazingira magumu na umasikini uliokithiri.

IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.