katiba mpya

Habel Chidawali, Mwananchi

Dodoma. Watanzania wameaswa kuwa makini na kuukubali mfumo wa Serikali tatu kwani ndiyo pekee utakaoondoa malalamiko na kero za Muungano.

Mbali na hilo wametakiwa kukumbuka na kuzionea huruma fedha za walipa kodi ambazo zimetumika kulipa tume 45 na vikao 50 vilivyoketi kujadili kero za Muungano kwa kipindi chote cha miaka 49 lakini hakuna mafanikio hadi sasa.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mjumbe wa Baraza la Katiba Ally Salehe wakati akitoa ufafanuzi kwa wajumbe kuhusu masuala ya Muungano ndani ya Katiba Mpya kwa wajumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ya Dodoma Mjini.

Mtazamo kuwa Serikali tatu ni kuongeza gharama si za kweli na badala yake ndiyo pekee sululisho la kuondoa kero zaidi ya 47 za Muungano ambazo zimedumu kwa muda mrefu.

Tatizo la Muungano lilianzia mwanzo muda mfupi baada ya nchi hizo mbili kuungana licha ya kuwa hakuna Watanzania ambao wamewahi kuulizwa mustabali mzima wa Muungano ndiyo maana tume iliona ni vema kuliweka katika Katiba Mpya.

Mfumo wa Muungano huo ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 49 bado una mambo ambayo yamefichika na kutolea mifano ya baadhi ya Mawaziri kuwa licha ya kuchapa kazi lakini upande wa pili wanaonekana kuwa hawafanyi kitu.

“Hebu fikiria hata Magufuli (Waziri wa Ujenzi) amejenga barabara ngapi Zanzibar, je huyu wa Wizara ya Afya amejenga Zahanati ngapi kule Zanzibar, lakini hawa wote wanaitwa ni Mawaziri na wanaingia katika Bunge la Muungano sasa hapa kama si kimvuli ni nini,” alihoji na kuongeza:..

Aliwakumbusha Watanzania kuwa inashangaza kuona Makamu wa Rais na Waziri wa kushuhulikia Muungano lakini hana mamlaka ya kuingia Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.