Imewekwa na Hamed Mazrouy

Mbunge Ubungo (Chadema), John Mnyika.

 

WABUNGE wa upinzani jana walizua tafrani bungeni na kusababisha kikao kilichokuwa kikiongozwa na Naibu Spika, Job Ndugai kuvu njika kabla ya muda uliokuwa umepangwa. Wabunge hao wa upinzani walisimama wote kwa pamoja na kuanza kupiga kelele za kupinga hatua ya Ndugai kuruhusu kujadiliwa kwa hoja ya Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe.

 

Profesa Maghembe katika hoja yake ambayo iliungwa mkono na wabunge wa CCM, alikuwa akipendekeza kuo ndolewa bungeni kwa hoja binafsi iliyokuwa imewasilishwa mapema na Mbunge Ubungo (Chadema), John Mnyika.
Mnyika katika hoja yake alikuwa akitaka Bunge lia zimie kuitaka Serikali ichukue hatua za haraka ya kuboresha upatikanaji wa majisafi na ushughulikiaji wa majitaka katika Jiji la Dar es Salaam.

 
Baada ya Ndugai kuruhusu hoja ya Profesa Maghembe kujadiliwa badala ya hoja ya Mnyika, wabunge wa upi nzani walisimama na kuanza kupiga kelele za kupinga kile walichodai kwamba ni Naibu Spika kuvunja kanuni ambazo anapaswa kuzisimamia Ilivyokuwa

Profesa Maghembe aliyekuwa mchangiaji wa kwa nza katika hoja ya Mnyika alitoa kauli kwamba Serikali inaendelea kukamilisha miradi mbalimbali ya maji jijini Dar es Salaam, hivyo kutaka hoja ya Mnyika iondolewe.
Kabla ya kutamka maneno hayo, tayari wabunge wa upinzani bila kujali vyama vyao walikuwa wameanza kumzomea na kupiga kelele kiasi kwamba maneno yake ya mwisho hayakusikika.
Baada ya hapo alisimama Naibu Spika na kuwataka wabunge watulie ili waanze kuchangia hoja hiyo na alimtaka Mnyika kuzungumza, lakini kabla ya Mnyika, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee alisemama na kuanza kuzungumza baada ya Naibu Spika kumruhusu.
“Mheshimiwa Naibu Spika naona mwendelezo wa uvunjwaji wa taratibu na kanuni za Bunge, hoja binafsi zinaratibiwa na kanuni ya 57 na 58,”alisema Mdee na kuongeza;
“Kanuni hizi mbili ukizisomaoi Waziri anatakiwa kueleza kipengele gani kitoke…….”
Kabla Mdee hajamaliza kueleza Naibu Spika, alisimama na kumtaka Mnyika achangie kama alikuwa ana la kusema, lakini akamkatisha na kelele zikaanza bungeni.
Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani, Tundu Lissu alisimama kutaka utaratibu, lakini Naibu Spika Ndugai alimkatisha kisha akasema “Waswahili wanasema kuchamba kwingi……”
“Wewe ni “Chief Whip” (Mnadhimu Mkuu) upande wa Serikali umetoa hoja na sisi tunachangia hivyo tunachangia sasa,” alisema Naibu Spika na kumwita Mdee aendelee kuchangia.
Hata hivyo, Mdee alikataa na Naibu Spika alimwita Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Zarina Madabida kuendelea kuchangia.

MWANANCHI

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.