Naibu Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Mh, Issa Haji Gavu akimsikiliza mfanya kazi wa kituo cha signal Tower cha AIS CM jinsi kinavyofanya kazi kutambua vyombo vilivyoko baharini. Kupitia chombo hicho ambacho kimefungwa hivi karibuni kina uwezo wa kutambua mwenendo wa meli na kama kuna ajali imetokea katika eneo la bahari ya Zanzibar. (Picha kwa hisani ya Mapara).

Naibu Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Mh, Issa Haji Gavu akimsikiliza mfanya kazi wa kituo cha signal Tower cha AIS CM jinsi kinavyofanya kazi kutambua vyombo vilivyoko baharini. Kupitia chombo hicho ambacho kimefungwa hivi karibuni kina uwezo wa kutambua mwenendo wa meli na kama kuna ajali imetokea katika eneo la bahari ya Zanzibar. (Picha kwa hisani ya Mapara).

 

Na Mwinyi Sadala.

Mfumo wa kufuatilia na kujua matukio ya ajali za meli baharini, umeanza kufanya kazi rasmi Zanzibar.

 

Mfumo huo umeanza kazi baada ya kazi kufunga chombo maalum cha kutoa taarifa za mwenedo wa meli zinapokuwa safarini  (AIS) kukamilika Saateni mjini hapa.

 

Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar, Issa Haji Gavu, jana alikagua mtambo unaofanyakazi ya kufuatilia safari za meli kwa kutumia mtandao wa mawasiliano.

 

Mfumo huo una uwezo wa kufuatilia safari za meli za kisasa ambazo hata hivyo, zitahitaji kufungwa vifaa  maalum vya kuunganisha mawasiliano na mfumo huo.

 

Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Bandari, Kapteni Makame Hassan,  alimweleza Waziri Gavu, kuwa pamoja na kujua ajali na kubainisha mahali zilipotokea na umbali wake kutoka bandarini mfumo huo, pia utabainisha matukio ya kiharamia.

 

Kuhusu aina ya vyombo vya usafiri vitakavyonufaika na mfumo huo, Kapteni Makame, alisema kwa sasa Kampuni ya Azam Marine Ltd ndiyo itakayonufaika sababu meli za kampuni hiyo zina vifaa vyenye uwezo wa kuunganisha mawasiliano moja kwa moja na mfumo huo.

 

Alisema kabla ya teknolojia hiyo ya mawasiliano, walikuwa wakitumia huduma za redio na wakati mwingine mawasiliano yalikuwa magumu kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

 

Waziri Gavu kwa upande wake, alisema baada ya kupatikana kwa mfumo huo, meli zote zinazofanya shughuli za uchukuzi visiwani humu, zitalazimika kuwa na chombo maalum cha kuwaunganisha na mfumo huo.

 

Hata hivyo, alisema Serikali Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), itatunga kanuni ambayo italazimisha vyombo hivyo kuwa na vifaa vya kuwaunganisha na mfumo huo katika mali zao.

 

Gavu alisema kanuni hizo zitatungwa baada ya Rais wa Zanzibar, kusaini Muswada wa Marekebisho ya Sheria Usafiri Baharini ya mwaka 2006 iliyofanywa  marekebisho na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Januari, mwaka huu.

 

“Chombo hiki cha kufuatilia mwenendo wa meli kina umuhimu mkubwa katika kurahisisha shughuli za uokoaji na kukabiliana na vitendo vya uharamia,” alisema Gavu.

 

Alisema chombo hicho cha mawasiliano kupitia mtandao, kinaonyesha mwenendo wa meli kama ipo salama na umbali wakati kikisafiri na wahusika ndani ya meli kubadilisha taarifa kupitia mawasiliano ya mtandao kupitia mfumo huo.

 

Alisema mtambo huo wenye thamani ya mamilioni ya fedha, umetolewa msaada na Serikali ya Ufarassa chini ya mpango wa kudhibiti usalama katika ukanda wa magharibi mwa Bahari ya Hindi na kusimamiwa na Shirikisho la Usafiri wa Baharini Duniani (IMO).

 

Gavu alizitaja nchi zilizonufaika na mpango huo kuwa ni Tanzania bara na visiwani, Mauritius, Seychelles, Msumbiji na Kenya.

 

“Mfumo wa mawasiliano wa AIS unasadia kutoa taarifa halisi za mwenedo wa meli baharini,” alisema Naibu Waziri Gavu.

One thought on “MTAMBO WA KUFUATILIA SAFARI ZA MELI WAANZA KAZI Z,BAR”

  1. kwa ninavyoijua serekali ya watu wenye akili zinazowatosha wenyewe hii, subiri computer iingie virus tu, or anything that kcan harm windows, Wallahi waweza kaaa ata miezi bila ya service! wala hawashughulishwi na VIFO vilivyoteokea, am saying threw experience, and i swear to GOD. hawa ni wazembe wa mwisho, halafu ni hatari sana

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.