Imewekwa na Hamed Mazrouy

Nembo ya shirika linalo husiana na elimu ya sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Bi. Irina Bokova amewasili leo Zanzíbar kwa ziara rasmi ya siku mbili.

 

Mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Amani Karume Bi.Bokova amepokelewa na Mwenyeji wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzíbar Ali Juma Shamuhuna.

 

Kwa mujibu wa Ratiba ya ziara yake Bi.Bokova atafanya atatembelea maeneo mbali mbali ya Mji Mkongwe ikiwa ni pamoja na kukagua Jengo la Makumbusho kuu ya Taifa ambalo lilianguka katika siku za karibuni.

 

Kesho Bi.Bokova atakuwa na Mazungumzo na Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzíbar wanaohusiana na Ofisi yake ikiwemo Waziri wa Wazira ya Elimu, Waziri wa habari Utamaduni Utalii na Michezo, Waziri wa Ustawi wa Jamii maendeleo ya Wanawake na Watoto na Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nishati katika Hoteli ya Serena mjini Zanzibar.

 

Aidha Bi. Bokova baada ya Mazungumzo hayo anatarajiwa kufanya Mkutano na Waandishi wa habarí kuhusiana na ziara yake.

 

Mkurugenzi huyo wa UNESCO atahitimisha ziara yake kwa kumtembelea Rais wa Zanzíbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein Ofisini kwake.

 

IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.