Imewekwa na Mhammed Khamis

 

Jaji mkuu wa Zanzibar Mh, Omar Othman Makungu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mahakama ya watoto hapa Zanzibar uzinduzi huo.
Jaji mkuu wa Zanzibar Mh, Omar Othman Makungu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mahakama ya watoto hapa Zanzibar uzinduzi huo.

JAJI MKUU WA ZANZIBAR MH OMAR OTHMAN MAKUNGU AMESEMA KUANZISHWA KWA MAHAKAMA YA WATOTO NCHINI KUTASAIDIA KUPUNGUZA MRUNDIKANO WA KESI KATIKA MAHAKAMA YA MKOA.

AMESEMA MAHAKAMA HIYO ITAKUWA NA JUKUMU LA KUSHUGHULIKIA KESI ZA JINAI ZINAZO HUSU WATOTO WALIOCHINI YA UMRI WA MIAKA 18 IKIWA NI UTEKELEZAJI WA SHERIA NAMBA SITA YA MWAKA 2011 YA SHERIA YA MTOTO  ZANZIBAR .

MH MAKUNGU AMEYASEMA HAYO KATIKA UZINDUZI WA MAHAKAMA HIYO ULIYOFANYIKA MAHAKAMA KUU ZANZIBAR VUGA.

  AMESEMA LENGO LA KUANZISHWA KWA MAHAKAMA HIYO NI KUTOA HAKI ZINAZOSTAHILI KWA WATOTO KUTOKANA NA KUONGEZEKA KWA VITENDO VYA UDHALILISHAJI WANAVYOFANYIWA.

 AIDHA MH MAKUNGU AMESEMA MAHAKAMA HIYO IMEANDAA MAZINGIRA RAFIKI YATAKAYO MUWEZESHA MTOTO KUJIELEZA KWA UFASAHA WAKATI WA UENDESHWAJI WA KESI HIZO MAHAKAMANI.

  NAE KATIBU MKUU  WIZARA YA USTAWI WA JAMII MAENDELEO YA WANAWAKE NA WATOTO BI FATMA GHARIB BILAL AMEWATAKA WANANCHI KUZITUMIA MAHAKAMA HIZO KWA KUPELEKA KESI ZINAZO WAHUSU WATOTO ILI KUONDOKANA NA MATATIZO YANAYOWAKABILI.

MAPEMA MKURUGENZI WA KITUO CHA HUDUMA ZA SHERIA ZANZIBAR BI, MWANAHARUSI MIRAJI AMEAHIDI KUWA KITUO HICHO KITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA MAKUNDI  MBALIMBALI ILI KUTOA TAALUMA JUU YA UMUHIMU WA MAHKAMA HIYO ILI IWEZE KUFANYA KAZI ZAKE KWA UFANISI.

 JUMLA YA DOLA ZA KIMAREKANI ELFU TANO  ZIMETUMIKA KATIKA UJENZI WA MAHAKAMA HIYO KWA UFADHILI WA SWEDEN .

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.