Imewekwa na Hamed Mazrouy

 

Vitendo vya unyanyasaji na ubakaji kwa Wananwake ni miongoni mwa matendo yanayorudisha nyuma harakati za maendeleo Nchini hususani kwa Wanawake ambao ni miongoni mwa nguvu kazi ya Taifa.

Hayo yamekuja  kufuatia kukithiri kwa matendo ya Ubakaji na unyanyasaji Wananwake huko katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.

 

Wananchi mbali mbali wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wamesema kuwa bila ya kudhibitiwa vitendo vya unyanyasaji na ubakaji ndani ya Mkoa huo kutakuwa hakukaliki kutokana na kukithiri kwa vitendo hivo siku hadi siku na kupelekea kuwepo kwa hofu kubwa kwa wakaazi wa Mkoa huo.

 

Wakielezea kuhusiana na maeneo yaliokithiri na vitendo hivyo vya ubakaji kwa sasa ni maeneo ya karibu na Bahari ya hindi ikiwemo  Nungwi,Pwani mchangani na baadhi ya Sehemu nyengine ndani ya Mkoa huo

 

Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa  Kaskazini Unguja amesema kuwa kukithiri kwa vitendo vya ubakaji ndani ya maeneo kadhaa yaliopo kwenye Mkoa wake yamekuja kutokana na ubadilikaji wa tabia kwa baadhi ya wananchi ndani ya jamii na ndio miongoni mwa jambo ambalo linasababisha kuwepo kwa matatizo hayo ya ubakaji kwenye Mkoa huo.

 

Aidha ametoa wito kwa jamii kuzingatia zaidi mila la desturi zao na sio kuiga mambo yasioenda na jamii husika kimaadili,kwani kufanya hivo kutaweza kusaidia kupunguza au kuondosha kabisa matatizo hayo.

 

 

KWA MSAADA WA HABARI ZA MAWIO

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.