Imewekwa na Hamed Mazrouy
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema ipo katika mpango wa kutafuta nishati mbadala ya umeme ili kuondoa utegemezi wa nishati moja.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wizara ya ardhi makaazi, maji na nishati Bw, Ali Khalil Mirza wakati wa utambulisho wa nishati mbadala ya jua na upepo uliofanywa na kampuni ya Solar wind limited ya Ujerumani huko katika ofisi ya wizara hiyo Forodhani .
Amesema serikali inakaribisha wawekezaji kutoka nchi tofauti katika uwekezaji wa nishati hiyo ambapo hadi sasa taasisi mbali mbali zimejitokeza kutoa mapendekezo ya uwekezaji.
Aidha amesema sheria ya nishati mbadala bado haijaanzishwa Zanzibar hata hivyo wizara hiyo inaangalia uwezekano wa kuanzisha sheria hiyo kwa maslahi ya wananchi wa zanzibar.
Nae Meneja wa kampuni ya Solar wind limited Bw, Joseph Gold kutoka Ujerumani amesema lengo la kampuni hiyo ni kutoa mchango wao kwa sekta ya nishati nchini ambayo imeleta mafanikio makubwa katika nchi nyengine.
Amesema kampuni hiyo ipo tayari kujenga mtambo wa mwanzo wa majaribio endapo watakubalika kuanzisha mradi huo.
hayo yawe ya kweli na yenye nia ya dhati na utendaji yakinifu
Nadhani hwenda ikawa nikweli kutokana na maelezo yao cha kufanya niluomba dua ili mwenyezimungu awape uwezo na nia yakutekeleza hili