Imewekwa na  hamed Mazrouy

Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa Cuf Juma Duni Haji akizungumza katika mkutano wa Hadhara wa Chama hicho.
Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa Cuf Juma Duni Haji akizungumza katika mkutano wa Hadhara wa Chama hicho.

Chama cha Wananchi CUF kupitia Mkurugenzi wake wa Habari Uwenezi na Mawasiliano ya Umma Mh:Salim Biman kimewataka wanachama wa chama hicho pamoja na wazanzibar wapenda maendele pamoja na Nchi yao kuwa watulivu pamoja na Mshikamano wa kuwa kitu kimoja sambamba na  kuacha tofauti ya vyama vyao badala yake waangalie maslahi ya nchi yao kwanza kitu ambacho kitaikomboa Zanziba na kuwa na Mamlaka kamili.

Kauli hio ya Mh:Biman  ametolewa leo katika Mkutano wa hadhara wa Chama hicho uliofanyika katika kiwanja cha Komba wapya ndani ya wilaya ya mjini Unguja na kuhudhuriwa na viongozi kadhaa wa juu ndani ya chama hicho pamoja na Wananchi mbali mbali waliokuwa wengi sana.

Nae mjumbe wa Baraza kuu Taifa CUF Mh:Ismail Jussa ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe amesema kuwa anashangazwa na baadhi ya watu wanaotamka hadharani kuwa wao wanao mkata halisi wa Muungano wa mwaka 1964 uliosisiwa rasmI na Mzee Karume pamoja na Nyerere .

Amesema kuwa kama kuna Mtu yoyote yule ambae ana hati halisi  ya Muungano japo kopi basi aioneshe hadharani ili iweze kuwatoa wasiwasi ambao kwa sasa umewajaa wazanzibar waliowengi sana kutokana na kudhulumiwa na Muungano huu uliopo hivi sasa ambao umeikandamiza Zanzibar kwa nyanja zote za kiuchumi.

Amefahamisha kuwa hapo miaka ya nyuma walijitokeza kundi la watu na kufungua kesi mahakamani ya  kudai hati halisi ya muungano huu na Mahakama kukiri kuwa imeshindwa kuwa na hati halisi ya Muungano wala  kopo yake ,lakini watu hao hawakuridhika ndipo walipoandikia barua UN kuwataka watoe uthibitisho wa kuwepo kwa muungano huu lakini na wao pia walijibu kuwa hawakuwa na uthibitisho wowote kuhusiana na muungano uliopo baina ya Zanzibar na Tanganyika hivo basi yanini kuendelea kuwepo kwa Muungano huu usiokuwa na uthibitisho wowote hule.

Nae Mjumbe wa Baraza kuu Taifa CUF ambae pia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii MH:Juma Duni Haji amesema kuwa anashangazwa sana kuwaona Wazanzibar wachache wakitaka kuwepo kwa Muungano huu wakati Watanganyika wenyewe kwa sasa wanataka Zanzibar iwe na  mamlaka kamili kitaifa na kimataifa iweje sisi wenyewe tusiungane na kuwa kitu kimoja kuitetea Nchi yetu.

Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa akihutubia katika mkutano wa hadhara
Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa akihutubia katika mkutano wa hadhara

Pia amefahamisha kuwa katika kipindi cha nyuma ilikuwa hakuna mzanzibar yoyote yule ambae aliweza hata kusubutu kuzungumzia kuhusu suala la Muungano lakini kwa sasa hali nikinyume na kila mtu anaweza kusema analolitaka kuhusu Muungano huu dhalim Kwa Zanzibar na ndio maana tunasema hadharani kuwa Muunagano huu hautufai.

Kuhusu suala la katiba ya Tanzania amesemea kuwa katiba hio haiwahusu Wazanzibar kwani katiba hio uhalisia wake ni katiba ya  Tanganyika hivo basi sisi Wazanzibar tuna katiba yetu iweje tuifate katiba ya kwao wakati ina katiba yake halisi.

Akizungumzia kuhusu suala la uendeshwaji wa Nchi hii ndani ya miaka mingi iliopita huko nyuma amesema kuwa nchi hii ilikuwa haiendeshwi kikatiba badala yake ilikuwa ikiendeshwa na Kanuni za Mwalimu Nyerere kwani alikuwa akiamua analolitaka yeye tu na sio kufuata katiba ambayo ndio  ilitakiwa ifuatwe kama ilivosheria ya Nchi kuwa ni lazima katiba ndio iwe muongozo ndani ya nchi hayo yamethibitishwa na hata aliekuwa Spika mstaafu wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano Pius Msekwa.

Amefahamisha kuwa lilipokuja suala la kuanzisha Benk kuu ya Tanzania (BOT) Tanganyika walikwenda kudai pesa za kufungulia benk kwenye Umoja wa Afrika Mashariki ambapo wahusika walikataa kuzitoa kutokana na kuwepo kwa majina ya Nchi mbili tofauti nazo ni Zanzibar na Tanganyika hivo basi kulipaswa kuwe na makubaliano kabla kati ya pande hizo mbili ndio wao waweze kuzitoa pesa hizo.

Kutokana na masharti hayo waliopewa ndipo Tanganyika wakatumia ujanja wao wa kuingiza suala la Sarafu kuwa mambo ya Muungano kwa lengo la kuzichukua pesa za Zanzibar ili waweze kuongezea na kufungua Benk kuu ambapo uanzishwaji wa Benk hio Zanzibar ilikuwa na kiasi ya asilimia 11.2 leo hii tunaambiwa Zanzibar haihusikia na haina shea ndani ya benk hio.

Aidha Mh:Duni amesema kuwa Nyerere alikuwa akikiogopa sana chama kilichokuwepo Zanzibar (ASP) na ndio maana akakiingigiza chama cha Tanu kuwa ndio chama ambacho kitaendesha Serikali na ikapitishwa sheria bila ya Wazanzibar wenyewe kujua kuwa chama cha Tanu ndicho kinachoongoza Serikali ya Muungano.

Sambamba na hayo amesema kuwa wananchokifanya CUF sasa sio kuvunja Muungano bali ni kudai haki yao ya msingi kisheria  kwani kama ni kuvunja muungano tayari ulishavunjwa na Nyerere tokea zamani  na sasa wanachokifanya wao ni kudai Nchi yao tu sio kama wanavosema baadhi ya watu kuwa wanantaka kuuvunja Muungano.

Aliendelea kwa kusema ikiwa Nyerere ametufikisha hapa tulipo sasa Wazanzibar nataka niwaulize ninani mnadhani atakae kaa Rais Tanganyika na kutujali Wazanzibar kama sio sisi wenyewe kudai Nchi yetu na muda wenyewe wakudai ndio huu tulionao sasa.

Amebainisha kuwa katika chaguzi mkuu unaokuja inshallah tukiwa hai basi hatuwezi kwenda na mfumo huu uliopo sasa wa katiba isipokuwa tutakwenda tukiwa ndani ya Mkataba kwani ndio suluhishi pekee lililobaki kwa nchi yetu

2 thoughts on “DUNI ASHANGWAZWA NA WAZANZIBAR WACHACHE WANAONGANGANIA KUWEPO KWA MUUNGANO”

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.