Imewekwa na Hamed Mazrouy

 

Watoto wenye Umri mdogo wakijishughulisha na ajira mbali mbali ili kuweza kujikimu kimaisha huku wakikosa hudumu muhimu ya Elimu.
Watoto wenye Umri mdogo wakijishughulisha na ajira mbali mbali ili kuweza kujikimu kimaisha huku wakikosa hudumu muhimu ya Elimu.

Mwakilishi wa shirika la kimataifa la kuhudumia watoto kanda ya zanzibar  Nd, Mubarak Maaman  amesema shirika hilo lina mpango wa kutokomeza ajira mbaya kwa watoto kwa kuweka mipaka itakayowafanya watoto hao waendelee na masomo.

 

Akifunga mafunzo kwa Wandishi wa habari wa vyombo mbalimbali huko ukumbi wa elimu mbadala Rahaleo amesema, mpango huo utasaidia kupunguza ajira mbaya zinazopelekea madhara mbalimbali yanayoathiri kiwiliwili na akili .

 

Aidha amesema kuwa shirika la kuwahudumia watoto linafanya kazi ya kuwabadilisha tabia na kuwarejesha mashuleni watoto hao kwa kushirikiana na  serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na taasisi mbalmbali  kwa kuwapa ushauri nasaha.

 

 Nd, Mubarak amefahamisha kuwa katika mikakati ya mradi huo ni kuweka mahakama ya watoto ambayo itakuwa inashughulikia kesi za watoto waliochini ya umri miaka kumi nane.

 

 Nae mratibu wa kupambana na ajira mbaya kwa watoto kutoka wizara ya kazi uwezeshaji wananchi  kiuchumi  na ushirika  Bi Fatma Mussa Omar amesema katika kupunguza utumikishwaji wa watoto wanatarajia kupata  sheria ambayo itawawezesha kufanya uchunguzi na kuwatambua wenye kuwatumikisha watoto hao kwa  kuwachukulia hatua za kisheria .

 

Mradi wa huo unafadhiliqwa na umoja wa ulaya na utekelezajiwa wake unaendeshwa na shirika la kuwahudumia watoto kwa kushirikiana na TAMWA ,COWPZ,PIRO na KUKHAWA.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.