Imewekwa na Hamed Mazrouy

 

Mkuu wa Mkoa Kaskazini Pemba Dadi Faki Dadi
Mkuu wa Mkoa Kaskazini Pemba Dadi Faki Dadi

Mkuu wa mkoa wa kaskazini pemba Mh, Dadi Faki Dadi amewataka wahamasishaji wa maendeleo ya jamii kutoka jumuiya ya wanawake Mkoa wa Kaskazini Pemba  kuwaelimisha wananchi ili watambue umuhimu wa  kupambana na ukatili wanaofanyiwa wanawake na watoto.

 

 Hayo ameyasema huko shengejuu wilaya ya wete wakati wa hafla ya kukabidhi baiskeli 50 zenye thamani ya shilingi milioni sita na nusu kwa wahamasishaji maendeleo ya jamii zilizotolewa na jumuiya hiyo kwa ufadhili wa shirika la ACTIONAID.

 

Aidha amesema kuwa ni vyema wahamasishaji hao kuendelea kutoa taaluma ili kujenga uwelewa kwa jamii pamoja kutambua wajibu wao katika kutetea na kulinda haki za msingi za wanawake na watoto.

 

Mkuu huyo wa mkoa amesisitiza haja kwa wahamasishaji hao kuvitumia vyombo vya sheria katika kudai haki na kuacha tabia ya kusuluhisha migogoro inyojitokeza katika shehia zao.

 

Mapema mratibu wa mradi huo Bi Nadra Subeti Ali amesema kuwa mradi huo una lengo la kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake na watoto  na kuhakikisha kuwa haki zao za kulindwa na kuishi kwa amani na utulivu zinathaminiwa.

 

Na Mwandishi wetu Pemba

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.