Imewekwa na Hamed Mazrouy

 

Mama mmoja jina linahifadhiwa mkaazi wa  Makadara wilaya ya mjini Unguja  akumbwa na tatizo la kuungua moto baaada ya kumwagiwa mafuta na Mume wake wa ndoa huko nyumbani kwao Makadara usiku wa manane

 

Akieleza kuhusiana na mkasa mzima Mama huyo  amesema kuwa kitendo hicho

cha Mume wake kumpiga na kasha kumwagia mafuta kimekuja baada ya Mume huyo kucherewa kurudi nyumbani kwake ambapo amesema kuwa alirudi mnamo majira ya saa tisa usiku na kuanza kumlaumu mke wake kuwa amelala nje wakati yeye ndio alichelewa kurudi ndani ya nyumba hio.

 

Amesema kuwa kutokana na  mume wake kuwa na tabia ya kumpiga kila mara anaporudu usiku  na kumtolea maneno machafu ya kumkashifu kwa kumwita mke wake huyo kuwa ni Malaya jambo ambalo yeye mwenyewe binafsi halipendi na amechoka nalo.

 

Aidha mama huyo amefahamisha kuwa licha ya kutaka kujaribu kukimbia baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya lakini alishindwa kutokana na kudhibitiwa ndipo badae mume huyo akaanza kumpiga na kumwagia mafuta hatimae kumchoma moto na hadi sasa yupo katika Hospitali ya Al-rahma iliopo kilimana wilaya ya mjini Unguja.

 

 

Sambamba na hayo amesema kuwa kutokana na kuchoka na madhila anayopata kutoka kwa mume wake ameamua kua mara hii kutokukubali  na atahakikisha kuwa anafika katika vyombo husika ili hatuwaza kisheria zichukuliwe juu yake.

 

 

 

Kwa upande wake mume aliejitambuisha kwa jina moja tu la Mkadara amesema kuwa tatizo hilo ni miongoni mwa matatizo ya kawaida tu ndani ya nyumba na yanaweza kutokea muda wowote hule.

 

Pia amekataa kuhusika na tukio hilo analodai mke wake kuwa amefanyiwa isipokuwa anasema kuwa yeye hakumchoma moto ila alijichoma mwenyewe kwa bahati mbaya.

 

CHANZO HABARI ZA MAWIO.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.