Imewekwa na Hamed Mazrouy

 

JAJI MKUU WA ZANZIBAR MH. OMAR OTHMAN MAKUNGU
JAJI MKUU WA ZANZIBAR MH. OMAR OTHMAN MAKUNGU

Jaji mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu amesema vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia bado ni tatizo kubwa kwa Zanzibar kutokana na Elimu ndogo kwa wananchi.

 

Mh. makungu amesema hayo alipokuwa kizungumza na wandishi wa habari huko Ofisini kwake vuga juu ya maadhimisho ya siku ya sheria february saba mwaka huu.

 

Amesema Mahakama Nchini zimekuwa na kesi nyingi za aina hiyo hasa za ubakaji dhidi ya Watoto hivyo elimu zaidi inahitajika kwa wananchi ili kupunguza vitendo hiyo.

 

Mh.  Makungu amesema katika kipindi cha Mwaka 2011 jumla ya kesi 77 kati ya hizo 34 zimetolewa uwamuzi, moja imepatikana na hatia na 33 wameachiwa huru.

 

 

Aidha amesema kuwa zaidi ya  kesi 43 zimeshindikana kusikilizwa kutokana na kukosa ushahidi.

 

kuhusiana na  maadhimisho ya siku ya sheria amesema lengo la siku hiyo ni kutoa elimu kwa Wananchi juu ya umuhimu wa kuripoti kesi za unyanyasi wa kijinsia  zinazotokea katika jamii.

 

Amesema Kuwa Ofisi yake inaendelea na mikakati ya kuimarisha utendaji wa m

ahakama hasa katika kutoa haki ili kurejesha imani juu ya utendaji wa mahakama hizo.

 

Sherehe za siku ya sheria zanzibar zinatarajiwa kufanyika katika viwanja vya bustani ya victoria na mgeni rasm anatarajiwa kuwa rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dr. Ali Mohammed Shein.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.