Imewekwa na Hamed Mazrouy

Watu ishirini na saba wanusurika kufa kufuatia ajali ya kuzama kwa Jahazi lilokuwa likitokea Tanga kuja Unguja usiku wa jana kuamkia leo.
Jahazi hilo lilikuwa na jumla ya watu thalathini na saba pamoja na mizigo mbali mbali ndani yake ikiwemo magunia ya bidhaa mbali mbali lilipinduka usiku wa jana majira ya saa nane za usiku kutokana na hali mbaya ya hewa.
Kwa mujibu wa Kamamnda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja Nd
:Ahmada Abdalla amethibitisha kutokea kwa tukio hilo usiku wa jana katika Bahari ya Mkokotoni ila amesema kuwa ajali hio imekuja kufuatia hali mbaya ya hewa kitu ambacho kimepelekea kutotambulika kwa ajali hio tokea jana hivo taarifa kamili kuhusu ajali hio imetambuliwa leo majira ya mchana.
Aidha amesema kuwa jitihada za uwokozi tayari zilichukuliwa na wavuvi wa NMkokotoni kupitia vyombo vyao vya baharini wakiwa kwenye harakati zao za uvuvi na hadi sasa kwa kushirikiana na Serikali bado wanaendelea na shughuli za uwokozi kwa ajili ya kuwatafuta watu wengine kumi waliokuwa hawajaonekana hadi hivi sasa.
Hivo ametowa wito kwa wananchi wajiepushe kusafiria vyombo ambavyo havijathibitishwa kwa ajili ya usafiri wa abiria kwani vinaweza kusababisha vifo visivotarajiwa.