MBUNGE mstaafu wa Kwela,Sumbawanga mkoani Ruvuma, Chrisant Mzindakaya ameitaka katiba ilinde Muungano, kwa madai kuwa ukivunjika madhara yake kwa usalama wa nchi ni makubwa kuliko bomu.

 

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam baada ya kuwasilisha maoni yake kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mzindakaya alisema kuwa hasara ya kuvunjika kwa Muungano ni kubwa kwani ni uhai wa taifa.

 

“Muungano ukivunjika tutatafutana hapa, kutakuwa na ugomvi na hasara itakayopatikana ni kubwa na nchi za Magharibi watafurahi maana watatugawa na hapo uvamizi wa rasilimali utazuka,” alisema.

 

Mzindakaya ambaye ameshika wadhifa wa ubunge kwa miaka 40, alisema kuwa amependekeza katiba mpya iandaliwe kwa maslahi ya nchi na kuitaka tume hiyo inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba, kutokubali maoni ya viongozi wanaotamani vyeo.

 

Alisema katiba hiyo iifanye nchi izaliwe upya ikiwemo rasilimali za nchi kuwa za Watanzania na mmiliki awe serikali.

 

“Ardhi, madini, gesi na maliasili zote zinaweza kuwekezwa, lakini wananchi wakamiliki asilimia 46, na lazima katiba ilinde wazalendo ili watu wasiwe watumwa katika nchi yao.

 

“Nimependekeza katiba ikatae biashara ya chumvi, maua eti mwekezaji katoka nje ya nchi, sasa sisi tufanye kazi gani? Nimetaka wawekezaji wasajiliwe,” alisema.

 

Alisema kuwa amependekeza rais asipewe nafasi ya kuchagua wabunge kumi wakiwemo wa viti maalumu, badala yake wapigiwe kura na si kuchaguana kama wafanyavyo sasa.

 

Naye Mbunge wa zamani wa Moshi Vijijini, Thomas Ngawaiya, amependekeza katiba mpya itamke wazi rasilimali za nchi ni mali ya wananchi na itamke mrabaha utakaotolewa kwa eneo husika lenye rasilimali hiyo, ili kuondoa migogoro kama ya gesi ya Mtwara na mafuta ya Pemba.

 

Ngawaiya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utawala Bora na Maendeleo (Cegodeta), alipendekeza kuondolewa kwa viti maalumu kwa sababu vinadumaza wanawake na kuchochea rushwa ya ngono ndani ya vyama vya siasa.

 

CHANZO TANZANIA DAIMA

8 thoughts on “MZINDAKAYA ASEMA MUUNGANO UKIVUNJIKA NI HATARI”

  1. Mheshimiwa Mbunge mstaafu hayo ni maoni yako lakini hujaweka wazi kwa nini iwe hatari kwa usalama wa nchi. Aidha rasilimali za nchi hii ni za Watanzania wote na kma zinamilikiwa na watu kwanini miaka 40 yako ya bungeni hujaliona unakuja kuliona leo. Aidha jenga hoja sio vitisho na hofu kwa wanaotaka mabadiliko. Usalama na Amani ya taifa hili utaendelea kuwepo hasa ikiwa Muungano utafanyiwa mabadiliko makubwa ya kumuondoa Bwana na Mtwana ama sote tuwe mabwana au sote tuwe Watwana sio kama tulivyo sasa.

    Mawazo yangu

  2. Huyu jamaa kakaa ubunge miaka 40 lakini bado akili zake za samaki ivi ana maana gani kusema kuwa jaji warioba asiyakubali maoni ya viongozi wanaotamani cheo ivi kuna kiongozi ambae hatamani cheo ? basi ungemwambia wazi kuwa maoni ayachakachuwe tuu kama ambavyo wamekusudia huyu mzee hana ishu

  3. Mzeee kakaa kwenye ubunge miaka 40 bado ana vision ile ile ya miaka 40 kwani resilimali atachukuwa nani? Rasilimali zote mnachukuwa wenyewe kwa wenyewe and then unataka kusingizia watu wa ulaya. Tunataka tupumue sasa hamtuambii chochote kile mpaka kieleweka sio

    1. Mzee huyu nadhani ndio wale wanaojua fika kuwa Zanzibar pindi ikiwa huru bila yakuwa na muungano huu uliopo sasa itapiga hatuwa zaidi kimandeleo na ndio maana kutokana na kuwa hili hawalitaki hutumia kila njia ili wahakikishe kuwa wazanzibar hawafanikiwi juu ya adhma yao waliyonayo ya kutaka Nchi yao ili waweze kujiendesha na kujikwamua kimaisha

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.