Imewekwa na Hamed Mazrouy

Watendaji wa jeshi la polisi nchini wameshauriwa kuendeelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi ili waweze kuungwa mkono na wananchi katika kulinda amani na utulivu wa nchi.

 

Ushauri huo,umetolewa na Mwakilishi wa jimbo la Uuzini Mh, Mohamed Raza wakati akikabidhi vifaa vya ujenzi na michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 5  kwa watendaji wa jeshi hilo huko makao makuu ya polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja Mahonda.

 

Mh, Raza amesema kuwa jeshi la polisi ni kiungo muhimu   cha kudumisha   amani katika jamii hivyo wanatakiwa kuzidisha juhudi  za kiutendaji katika utekelezaji wa  majukumu yao kwa uadilifu.

 

Aidha amefahamisha kuwa lengo la kutoa vifaa hivyo ni miongoni mwa kutekeleza  ahadi  alizozitoa kwa jeshi hilo ili kuhakikisha askari wanafanya kazi katika mazingira mazuri yatakayowasaidia kutoa huduma bora na endelevu kwa jamii.

 

Nae  Kamishna msaidizi wa polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja Ahmada  Abdallah Khamis ametoa shukrani zake kwa Mwakilishi huyo juu ya msaada alitoa na kuahidi kuwa utatumika kwa shughuli iliyokusudiwa  ili ofisi za jeshi hilo ziwe za kisasa zinazoendana na taswira ya askarin wake.

 

Pia amesema jeshi hilo limekuwa na ushirikiano mkubwa na wananchi katika kupambana na harakati mbalimbali za uharifu na matukio mengine ya uhalifu ili kuhakikisha zanzibar inazidi kuwa kitovu cha amani duniani.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.