Imewekwa na Hamed Mazrouy

Wodi ya Watoto katika Hospitali kuu ya Mnazi mmoja Zanzibar
Wodi ya Watoto katika Hospitali kuu ya Mnazi mmoja Zanzibar

Jumla ya watoto 70 wenye matatizo ya macho wanatarajia kupatiwa matibabu ya macho katika hosptali kuu ya mnazimmoja.

Matibabu hayo yatakayo chukua kipindi cha wiki moja yatajumuisha watoto kuanzia siku moja hadi miaka 15 ambapo watafanyiwa upauaji na huduma nyengine.

Mkuu wa kitengo cha macho Zanzibar Dk Slim Mohammed Mgeni amesema wagonjwa wengine kumi wenye matatizo zaidi ya macho watapelekwa hospitali ya Muhimbili Dar es salaam kwa uchunguzi wa kina.

Dk, Slim amefahamisha kuwa  mpango huo wa matibabu ya macho kwa watoto utaendelea kila mwaka na kuwataka wazee kutumia fursa hiyo kuwapeleka watoto wao kupatiwa matibabu hayo.

Nao wazazi wa watoto wanaopatiwa huduma hiyo wameshukuru hospitali ya Mnazimmoja kwa kushirikiana na madaktari wa Muhimbili kutoa matibabu hayo kwa watoto wao.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.