Imewekwa na Hamed Mazrouy

Serikali ya mapinduzi zanzibar imeanza kutekeleza mapendekezo ya kamati ya baraza la wawakilishi iliyoundwa kuchunguza utendaji wa baraza la manispaa kwa kumuondoa madarakani mkurugenzi na mhasibu wa baraza hilo .

 

Akiwasilisha ripoti ya utekelezaji huo Waziri wa nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk . Mwinyihaji Makame amesema Mkurugenzi wa Baraza hilo ameondolewa katika wadhifa wake na mhasibu amehamishiwa taasisi nyingine.

 

Amesema mbali na hatua hizo serikali pia imepeleka suala la watendaji hao katika Ofisi ya Mwanasheria mkuu kupata ushauri wa kuwachukulia hatua za  kisheria zaidi.

 

Aidha Dk, Mwinyihaji amesema serikali pia inapitia vielelezo vya aina ya makosa dhidi ya wafanyakazi waliotajwa kwenye kamati hiyo ili kuwachukulia hatua za kinidhamu.

 

Wakati huo huo serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeshauriwa kudhibiti vitendo vya rushwa na ubadhirifu wa mali katika taasisi za serikali na mashirika ya umma ili kuepuka hujuma znizo jitokeza katika taasisi hizo.

 

Akitoa majumuisho ya ripoti ya uchunguzi wa shirika la umeme. Mwenyekiti wa kamati ya kuchunguza na kudhibiti hesabu za serikali na mashirika ya umma Mh, Omar Ali Shehe amesema iwapo mapendekezo ya ripoti hiyo hayatafanyiwa kazi wananchi watapunguza imani kwa utendaji wa taasisi za serikali..

 

Ripoti hiyo ya uchunguzi yenye mapendekezo 14 imekabidhiwa kwa spika wa baraza la wawakilishi mh. Pandu Ameir Kificho kuiwasilisha serikalini kwa ajili ya hatua za utekelezaji.

 

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.