Imewekwa na Hamed Mazrouy

 

MWAKILISHI wa Jimbo la Magomeni (CCM), Salmin Awadh Salmin, amesema ameshagazwa na mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Shumbana Amani Karume, kuungiwa umeme bure na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO).

Alitoa tuhuma hizo wakati akichangia ripoti ya uchunguzi kuhusu ubadhirifu katika shirika hilo iliyowasilishwa na mwenyekiti Kamati ya Kuchunguza Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma, Ali Omar Shehe.

Awadh alisema kwamba kitendo cha kumuungia umeme bure mtoto huyo wa kiongozi mstaafu katika kitega uchumi chake ni kwenda kinyume na misingi ya utawala bora Zanzibar.

Alisema kwa mujibu wa ripoti ya PAC, mtoto huyo aliungiwa umeme bure na kutumika nguzo 31 kuvuta umeme kutoka umbali wa kilomita 2.5 wakati wananchi wanyonge wamekuwa wakitozwa gharama Zanzibar.

Alisema kwamba kitendo hicho lazima kipigwe vita kwa sababu kimelenga kuitafuna nchi na kuvuruga misingi ya utawala bora.

 

CHANZO TANZANIA DAIMA

 

12 thoughts on “MTOTO WA KARUME AILIPUA ZANZIBAR”

   1. Wewe kila kitu unajibu ahsante kwa mchango wako tu??? Hebu please be more professional with some additional inputs on constructive or proffessional critique. Kama baadhi ya haya yatakuwa hayapatikani ktk mijadala yako kwa kila mara kuitikia ahsante kwa mchango wako tu, basi nasikitika sana kukwambia kuwa hii blog yako itakuwa sio dyanamic ya watu kujadiliana kama vile ilivyo ktk jamii. Nilibahatika kuingia ktk blog moja juu ya masuala ya Uamsho na nilipata mijadala mizuri mno kutoka kwa Waandishi kama wewe hadi kujua ukweli wa Undani zaidi na kubadilisha mawazo yangu. This is what I call proffessionalism sio wewe muda wote unajibu ahsante kwa mchango wako ama wangu. Haya nijibu ahsante namie pia kwa huu mchango wangu. Nami nakwambia ahsante kwa kupokea maoni yangu kama msomaji wa taarifa unazoweka. Samahani kwa usumbufu.

    1. Sawa kaka inshallah tumeyachukua mawazo yako na nitaangaza kafanyia kazi kuanzia sasa tuzidi kupeana ushirikiano na ushauri zaidi kuhakikisha kuwa lengo la kila mmoja wetu linatimia

   2. Kumbe unafanya na moderation pia??? Ndio maana Uandishi wa Zanzibar unakosolewa kila siku kuanzia Zanzibar Leo hadi blogs maana naamini ni gazeti moja tu la sauti ya serikali lililopo na hizi blogs pia nazo zinafanyiwa The so called Free Press Moderation. Kila la kheir.

    1. Hapa kwa muono wako kaka kuna kipi kibaya kimefanyia na ukahisi hakistahiki kufanyika ili tukiondoe najua nipo hapa kwa ushirikiano wenu pia hivo napaswa kusikiliza mawazo yenu

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.