Wazee wasiojiweza picha hii sio halisi
Wazee wasiojiweza picha hii sio halisi

Licha ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kujitahidi kupiga hatuwa kaika kuwatatulia changamoto mbali mbali zinazowakabili wazee wasiojiweza hapa Nchini lakini bado kumekuwepo kwa changamoto kubwa ya kutokuwepo kwa majengo ya kutosha ya kuweza kuwatunza wazee hao.

 
Hayo yamekuja baada ya wazee hao kutembelewa na waandishi wa Habari huko kijijini kwao Zingwezingwe wilaya ya  kaskazini B  Unguja kwalengo la kutaka kujua mchakato mzima wa kimaisha katika mazingira yaliyowazunguka.

 
Wazee hao wamesema kuwa ni siku nyingi hivi sasa wamekuwa wakikabiliwa na kutokuwa na makaazi halisi ya kuishi hali ambayo inachingia kuwepo kwa ugumu wa maisha kwa wazee hao.

 
Mmoja miongoni mwa wazee hao amesema kuwa licha ya kukabiliwa na changamoto hio lakini pia kumekuwepo na baadhi ya changamoto nyengine kama vile ukosefu wa huduma za kijamii zikiwemo Chakula na Mavazi.

 
Hivo wazee hao wameiomba serikali kupitia wizara husika  kuwapatia misaada mbali mbali itakayowawezesha kujikimu kimaisha na kuweza kujiona ni miongoni mwa wazeee wenye furaha kama walivo wananchi wengine.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.