Imewekwa na Hamed Mazrouy

Shamba la mazao mbali mbali picha hii sio halisi
Shamba la mazao mbali mbali picha hii sio halisi

Licha ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kulitilia mkazo kwa kiasi kikubwa sula la kilimo kwa wananchi wa Zanzibar ili liweze kuwaendeleza wananchi wa Zanzibar na kuwakuza kiuchumi kwa maslahi yao na  Taifa kwa ujumla lakini hali haipo hivo kwa upande wawakulima wengine hapa nchini.

Wakulima wa mazao mabli mbali katika kijiji cha ukongoroni wilaya ya kati Unguja wamelalamikia sula la kuwepo kwa wanyama wa haribifu katika mashamba yao jambo ambalo linawarudisha nyuma katika upatikanaji wa kupiga hatuwa mbele za kimaendele kupitia secta ya kilimo.

Wameyem hayo wakati wakizungumza na waandishi wa habari huko kijijini kwao,  wakibainishaa baadhi ya mazao yanayoharibiwa vibaya na wanyama hao kuwa ni Kunde, mbrazi na baadhi ya mazao mengine ndani ya mashamba yao kitu ambacho kimekuwa kikiwapa ugumu na kuwarudisha nyuma kimaendeleo husasani msimo  huu wa kuwanza kwakilimo.

Wamebainisha kuwa miongoni mwa Wanyama wanaowaharibia mazao yao ni kama vile Nguruwe,kima  na wengineo, pia wamendelea kusema kuwa uharibifu unaofanywa na wanyama hao unazidi kuwakosesha kipato ambacho kingetokana na mazao hayo licha ya kujitahidi kufanya bidii ya kulinda mazao yao kwa kutumia mitego ya asili kama vile vigigi na mengineyo kwa lengo lakulinda mazao yao lakini jitihada hizo zimekuwa zikishindwa kutokana na kuzidi kwa wanyama ndani ya mashamba yao.

Aidha wakulima hao wameiomba Serikali kupia Mabwana Shamba kuwapatia watalamu hao kwani kuwepo kwao kutaweza kuwasaidi kuwapa ushauri wakulima hao ni njia gain za kutumia ili waweze kulinda mazao yao na Wanyama waharibifu.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.