Imewekwa na Hamed Mazrouy

 

Fukwe za bahari Zanzibar
Fukwe za bahari Zanzibar

 

Kukua kwa Secta ya Secta ya Utalii Nchini Zanzibar ni sababu moja wapo itakayochangia kuwepo kwa maendeleo kwa Serikali yenyewe na wananchi kwa ujumla.

 

Hayo yamekuja kufuatia mazungumzo maalumu baina ya Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na mipango ya maendeleo,Mh:Omar Yussuf Mzee na Raisi na mtendaji mkuu wa mtandao wa mahoteli wa Four season Duniani Bi:Katholeen Teylor huko katika uwanja wa Ndege wa kimataifa Zanzibar alipokuwa akiwasili rasmi nchini kwa ajili ya uwekezaji.

 

Raisi huyo amesema kuwa amekuja Zanzibar kwa lengo la kuwekeza na kuanzisha Hoteli kubwa ya kimataifa ambayo itakuwa ni hoteli ya mwanzo kujengwa ndani ya Africa Mashariki.

 

Pia amesema hoteli hio itajengwa  Pongwe na  itagharimu kiasi cha Dola 50 milioni na itakuwa ni kubwa na yakifahari ukilinganisha na Hoteli nyengine zote,hali ambayo itachochea kwa watalii wa daraja ya kwanza kuvutika zaidi na hoteli hio hatimae Kukua kwa Uchumi wa Taifa na wananchi kwa ujumla.

 

 

Nae waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na uchumi mipango na Maendeleo Mh:Omar Yussuf Mzee amesema Serikali ya Zanzibar imejiandaa kuhakikisha ujenzi wa Hoteli hio na amesisitiza kutoa ushirikiano wa hali na mali baina ya Serikali ya Zanzibar na mtandao huo.

 

Sambamba na hayo amewataka wananchi kudumisha amani na kuondosha yale yote ambayo yanayoweza kuipelekea Zanzibar katika taaswira mbaya ili kuzidisha kiwango cha wawekezaji Nchini.

 

Four Season ni mtandao unaoenesha ujenzi wa mahoteli zenye hadhi na viwango vya kimataifa zinazofikia jumla ya Hoteli 91 katika nchi mbali mbali Duniani ikiwemo Bara Ulaya,Masariki ya kati na baadhi ya Nchi za Africa.

2 thoughts on “HOTELI YENYE HADHI YA KIPEKEE AFRKA MASHARIKI NZIMA ITARAJIWA KUJENGWA HIVI KARIBUNI ZANZIBAR”

  1. Kila siku mahoteli yanajengwa zanzibar lakini hayana faida yoyote kwa mzanzibar ajira hawapewi wanaofadika ni wakenya na wabongo tu eti kisingizio wazanzibar hawajasoma

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.