Imewekwa na Hamed Mazrouy

Picha hiii sio halisi
Picha hiii sio halisi

Wananchi mbali mbali waliojiunga na vikundi vya ushirika katika shehia ya Shumba Mkoa wa Kaskazini Pemba wawataka viongozi wao wa jimbo kuwatembelea kwa lengo la kupata kujua changamoto zinazowakabili ndani ya Shehia yao pamoja na kutafuta njia mbadala ya ya ufumbuzi wa changamoto hizo.

Wananchi hao wameyasema hayo huko kijijini kwao Shumba wakati wakizungumza na mwandishi wa habari hizi wamesema kuwa miongoni mwa changamoto ambazo zinakwamisha maendeleo yao katika secta ya kilimo ni pamoja na ukosefu wa mbegu pamoja na soko la kuuuzia bidhaa zao wanazopanda ambapo viongozi wa jimbo hilo wameshindwa kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo.

Aidha wamesema kuwa licha yakuwa  changamoto hizo wameshazieleza  mara kwa mara kwa viongozo wa jimbo hilo lakini chakushangaza wameshindwa kuzitatua kama walivowaahidi wakati wa kampeni za kutaka kuchaguliwa uongozi huo wakati walipokuwa wakiomba kura.

Wananchi hao wameendelea kubainisha kwa kusema tayari wameshawaita viongozi hao lakini bado hadi leo ii changamoto hizo hazijapatiwa ufumbuzi,  tatizo hilo kwa hio wanawaomba viongozi hao pamoja na viongozi wengine wa serikali wafike ndani ya maeneo yao ili waweze kuona changamoto zinazowakabili wapate kuwasaidia na kuwafanya waweze kujikwamua kimaisha.

CHANZO HABARI ZA MAWIO

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.