WATU wanane wameuawa na wengine kumi na moja kujeruhiwa kutokana na vurugu zilizizotokea jana mkoani Mtwara na Itete wilayani Ulanga, mkoani Mororgoro.

Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya Wilaya ya Masasi, Mkomaindo, Amima Simbo alithibitisha vifo vya watu saba waliofikishwa hospitalini hapo.

Kwa mujibu wa muuguzi huyo, maiti zilizopokelewa hospitalini hapo zilionekana zikiwa na matundu yanayodhaniwa kuwa ni ya risasi, baadhi yao kichwani, begani, viunoni na tumboni.
Aidha majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo pia walikuwa na majeraha mbalimbali ikiwamo ya risari.

Habari zaidi zinaeleza kuwa vurugu hizo zilizuka baada ya kundi la waandamaji, wengi wakiwa vijana waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda waliokuwa wakipinga mwenzao kukamatwa na kutaka kuvamia Kituo cha Polisi ili kumwokoa.

Vurugu hizo ziliendelea kuutikisa Mkoa wa Mtwara kwa siku ya pili mfululizo na kuutikisa Mkoa wa Mtwara, baada ya vurugu nyingine kuibuka wilayani Masasi jana.

Habari zinasema mbali na vifo na majeruhi, nyumba za wabunge wawili wa wilaya hiyo zimechomwa moto, ambapo pia magari, trekta, Ofisi za CCM Wilaya na Ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya ziliharibiwa kwa kuchomwa moto.

Wabunge ambao nyumba zao zimemwa moto ni Mariam Kasembe wa Masasi Mjini na Anna Abdallah Mbunge wa Viti Maalumu wilayani humo.

Juzi vurugu hizo zilitokea katika Mikoa ya Morogoro kati ya wakulima na wafugaji na kusababisha kifo cha mtu mmoja wakati mkoani Mtwara wananchi  wa eneo la Chikongola waliizingira nyumba ya diwani wa Kata ya Mikindani, Mohamedi Chehako kwa madai ya kuwahifadhi wachawi ndani ya nyumba yake.

Katika vurugu hizo polisi walilazimika kutumia silaha yakiwamo mabomu ya machozi ili kupoza hali ya hewa, ambapo nyumba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia ilichomwa moto.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili kuhusu vurugu hizo, Mbunge wa Masasi Mjini, Mariam Kasembe alisema kuwa nyumba yake iliyoko Masasi mjini imechomwa moto na kuteketea kabisa, huku mali zikiibwa na kwamba familia yake sasa haina makazi.

Aliongeza kwamba mbali na uharibifu, vurugu hizo zimesababisha pia mama yake mzazi kukimbia na mpaka sasa hajulikani alipo.

“Wamechoma trekta na gari lililokuwepo nyumbani kwangu, watoto wangu na mume wangu walipoona hali hiyo wakakimbia,” alisema Kasembe akieleza kuwa hawezi kuthibitisha chanzo cha vurugu hizo, lakini anahisi kuwa zinatokana na mgogoro wa gesi.

CHANZO MWANACHI

2 thoughts on “GESI SASA YASABABISHA MAUWAJI NA KUJERUHI KADHAA MTWARA”

 1. Salam kwa ndugu zangu wakizanzibar

  Umefika wakati sasa wakuipata nchi yetu maana kama vile mtwara walivypewa gesi yao na sisi wazanzibar tuna haki ya kupewa Nchi yetu ikiwa kwa bunduki, virungu, mabomu au amani lkn mpk tupate NChi yetu.

  Ushauri:
  Wakati muheshimiwa amesema mkataba wamuungano anao tufanyeni hima kabla hajageza maneno yake atuoneshe.

  Maana hapo ndipo pakuwanzia kwa vyovyote vile km upo au haupo basi hapo ndipo pakuanzia

  Ndugu wawakilish wetu tunawaomba mupeleke hoja binfsi siku ya tarehe 3 April 2013 kwenye baraza la Wawakilishi kudai hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. kama alivyosibitisha Dr. Shein kuwa anao Ikulu basi na atuoneshe.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.