
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed amesema kuwa kuekeza katika shopping more itakuwa kivutio kikubwa kwa watu mbali mbali na kuweza kukuza uchumi nakuondokana na umasikini nchini.
Aliyasema hayo huko katika Ofisini kwake vunga Zanzibari wakati akiwa na mazungumzo na kampuni ya (ANHU)Group co,LTD ya China.
Aidha alisema kuwa Zanzíbar inania ya kuekeza katika sekta ya utalii kwani sekta hiyo ndiyo inayoweza kukuza uchumi wa nchi .
Alieleza kuwa waekezaji hao wataweza kuekeza Zanzíbar mpaka waweze kufanya utafiti wa maeneo ambayo wanatarajia kuekeza ili waweze kuridhika nayo kwa biashara .
Waziri huyo amesema kuwa kampuni hiyo imeweza kuekeza sehemu Mbali Mbali za kimataifa pamoja na África mashariki ikiwemo Zimbabwe na Muzambiq.
Alifahamisha kuwa katika nchi yetu ya Zanzíbar tunategemea zaidi uchumi wetu kwa njia ya utalii ikiwa wawekezaji wa kampuni hiyo wataekeza wataisaidia serikali kuengeza pato kutokana na kivutio kwa kitalii.
“Utalii ni kiungo kikubwa kwa serikali” alisema Abuod.
Alisema kuwa kampuni mbali mbali ambazo zinataka kuekeza Zanzíbar kwa kushajihisha maeneo mengine tofauti Serikali haina pingamizi kwani inaunga mkono jitihada za Serikali.
Pia alifahamisha iwapo wawekezaji wataekeza Zanzíbar wananchi watafaidika kwa kuweza kupata ajira nchini mwao .