Imewekwa na Hamed Mazrouy

Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii imesema kua suala la kuifanya hospitali ya Mnazi Mmoja kua ya rufaa ni suala la muda mrefu kuweza kufikiwa hivyo kunahitajika matayarisho mbali mbali ili kuweza kufikia hatua hiyo.

Akijibu swali katika kikao cha baraza la Wawakilishi Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dk, Sira Ubwa Mamboya  amesem Wizara ya afya imeanza matayarisho ya ujenzi wa jengo jipya pembezoni mwa hospitali hiyo ili kuhamishia baadhi ya huduma zinazotolewa ili kutoa nafasi ya kuifanya hospitali hiyo kuwa ya rufaa.

Amesema matayarisho mengine yanayofanywa ni kutafuta kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa hospitali kubwa  kwa ajili ya kuhamishia shughuli nyengine zitakazo ondoshwa katika hospitali ya Mnazi mmoja.

Pia amesema kuwa Wizara imeandaa utaratibu wa kuwasomesha wafanyakazi watakao toa huduma za ziada na tayari baadhi ya wafanya kazi wameshapelekwa kusoma na wengine wanaandaliwa kupelekwa masomoni.

Maandalizi mengine ambayo tayari yamefanyika ni kujua maradhi ya yanayotakiwa yatibiwe kwa ripoti za wagonjwa wanaohudhuria katika mahospitali kwa ajili ya matibabu ya maradhi hayo.

Dk, Sira amesema kuwa huduma zinazotakiwa kutolewa kwenye hospitali ya rufaa ni za maradhi ya Saratani, Operesheni za moyo, matibabu ya mafigo, usafishaji wa damu pamoja na kitengo cha ajali na dharura.

Huduma nyengine zitakazo tolewa ni pamoja na rufaa kwa mama wajazito na watoto, kitengo cha upasuaji wa maradhi ya mishipa ya fahamu na vichwa maji kwa watoto pamoja na kitengo cha idara ya meno kufanya upasuaji wa midomo sungura, taya na shingo kwa kutumia TV maalum pamoja na mashine za kisasa katika kitengo cha macho ambazo zitatumika kupima vipimo vyote vitakavyo hitajika kulingana na huduma zitakazo hitajika.

2 thoughts on “Hospitali ya Mnazi Mmoja kuwa hoispitali ya dharura.”

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.