Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar

izara ya miundo mbinu na mawasiliano inakusudia kulifanya shirika jipya la meli la Zanzibar kujitegemea ili kuingia katika ushindani wa kibiashara na mashirika mengine ulimwenguni.

Hayo yameelezwa na waziri wa wizara hiyo mhe, Rashid Seif Suleiman alipokuwa akijibu hoja za wajumbe wa baraza la wawakilishi waliochangia mswada wa sheria ya kuanzishwa shirika jipya la meli Zanzibar.

Amesema mswaada wa sheria hiyo itarejesha shirika hilo kujitegemea na kuendeshwa kwa faida na kutoa huduima bora kwa wananchi.

Amesema bodi ya uendeshaji wa shirika hilo utajumuisha wajumbe kutoka sekta binafsi ili kuweza kuliendesha kwa umakini zaidi.

Aidha amesema kuwa kutakuwepo na meli zinazo milikiwa na serikali kwa ajili ya kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria pamoja na mizigo ili kutoa unafuu wa bei za nauli kwa wananchi ili waweze kumudu gharama za usafiri.

Wajumbe wa baraza hilo wameukubali na kuupitisha mswaada huo na kuwa sheria .

 

Wakati huo huo Waziri wa nchi ofisi ya rais na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk, Mwinyihaji Makame samesema utoji wa huduma za dharura kama zimamoto na uokozi umefikia hatua mzuri katika awamu ya 2010-2015.

Amesema vituo vipya vya huduma ya zima moto ngazi ya wilaya vimeanza kujengwa na kuwapatia magari saba ya kuzimia moto na mawili ya kubebea wagonjwa.

Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi Dk, Mwinyihaji Makame amesema jumla ya vituo vitatu vimeanzishwa na kupatiwa huduma katika maeneo ya mwanakwerekwe,  bandari ya malindi na bandari ya mkoani.

Aidha amesema hatua ya ujenzi wa kituo cha marumbi wilaya ya kati umeanza na utaratibu unaendelea wa kutafuta eneo jengine katika eneo la wete pamoja na wilaya nyengine ambazo huduma hizo hazipo.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.