Na Hamed Mazrouy

 WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI MH. OMAR YUSSUF MZEE
WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI MH. OMAR YUSSUF MZEE

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR IMESEMA HAINA TAARIFA ZA WANANCHI WALIOSUSIA KAZI ZA SENSA WALIPIGWA NA KUSUMBULIWA NA VYOMBO VYA DOLA.

AKIJIBU SUALA KATIKA KIKAO CHA BARAZA LA WAWAKILISHI WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI MH. OMAR YUSSUF MZEE AMESEMA TAASISI ZA SHERIA HAZIJAPOKEA MADAI YOYTE YA AINA HIYO.

AMESEMA BAADHI YA WANANCHI WALIOSUSIA KAZI HIZO NDIO

WALIOFANYA FUJO KWA KUWAPIGA NA KUWAKEJELI MAKARANI WA SENSA PAMOJA NA KUHARIBU GARI ZA SERIKALI.

MH. MZEE AMESEMA KATIKA MUDA WOTE HUO SERIKALI ILOICHUKUA BUSARA NA HEKIMA KWA KUJIEPUSHA KUTUMIA NGUVU.

AMEFAHAMISHA SERIKALI ILIWATUMIA VIONGOZI WA DINI NA WATU MASHUHURI KUWAELIMISHA WANANCHI UMUHIMU WA SENSA BADALA YA KUWACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.

HATA HIVYO WAZIRI MZEE AMESEMA TAKWIMU ZA WATU WALIOSUSIA SENSA ZILIPATIKANA KUPITIA OFISI ZA MASHEHA.

One thought on “Hakuna mtu aliepigwa kwa sababu ya kukataa kuhesabiwa-Omar Yussuf Mzee”

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.