Mkuu wa Mkoa ahimiza mashirikiano katika ulinzi.

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharib Mh;Abdalla Meinyi
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharib Mh;Abdalla Meinyi

Magharibi Mh, Abdalla Mwinyi Khamis amesema umuhimu wa ushirikiano,mahusiano na ubia katika kudumisha usalama ni kuleta maendeleo endelevu katika nchi.

Mh Abdalla ameyasema hayo alipoluwa akizungumza na wananchi wa Shehia ya Kianga katika kukabidhi mashine ya kufyatulia matofali kwa kikundi cha ulinzi shirikishi cha shehia hiyo

Amesema kuwa maendeleo endelevu hayapatikani pasipokuwa na amani kwa kutambua hivyo wananchi wa shehia hiyo wamekubali kushirikiana na jeshi la polis kufanya ubia wa kuondoa vitendo viouvu vinavyo hatarisha amani ili paweze kupatikana amani ya kudumu.

Kwa upande wake Kamishna wa Polisi zanzibar Bw Muasa Ali Mussa amesema mashine hiyo ya kufyatulia matofali yenye thamani ya zaidi ya shliingi laki tatu na vifaa vya kuanzia mradi huo ni msaada wa jeshi la Polisi kwa kikundi hicho na lengo ni kuwaendeleza kiuchumi baada ya kufanikiwa kuweka amani katika shehia hiyo

Nae mkuu wa wilaya ya Magharibi Bw Hassan Mussa Takrima amesema Polisi jamii imesaidia sana kupunguza kero za uhalifu katika wilaya hiyo hasa shehia ya kianga hivyo amewatka masheha wote kuanzisha mpango wa Polisi jamii ili kuweza kudhibiti vitendo vya kihalifu.

Akitoa shukrani mdau wa Polis jamii Kianga Bw Ahmed Ali amrani amelipongeza jeshi la Polisi kwa kuwapatia msaada huo na kuahidi kutumika kwa maslahi ya wanajamii ya kianga.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.