Naibu Waziri wa Ardhi,Makazi,Maji na Nishati Haji Mwadini Makame akipuliza filimbi kuonyesha ishara ya kuanza kwa mashindano hayo.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Naibu Waziri wa Ardhi,Makazi,Maji na Nishati Haji Mwadini Makame akipuliza filimbi kuonyesha ishara ya kuanza kwa mashindano hayo.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

Naibu Waziri wa Ardhi Makazi, Maji na Nishati Haji Mwadini Makame amewataka Manahodha wa Ngarawa waendelee kudumisha utamaduni wao wa kufanya mashindano ya Resi za Ngalawa kila ifikapo nuda wa maadhimisho ya shererhe za Mapinduzi ya Zanzibar. 

Wito huo aliutoa jioni ya jana wakati alipokuwa akitoa nasaha zake kwa Manahodha walioshiriki mashindano hayo huko Forodha Mchanga Mjini Zanzibar ikiwa ni shamra shamra za kutimiza miaka 49 ya Mapinduzi Zanzibar. 

Alisema kuwa Resi za Ngarawa ni moja ya utamaduni wa Zanzibar hivyo ipo haja ya kuenziwa mchezo huo ili kukuza utamaduni na kudumisha Mapinduzi ya Zanzibar yaliyo wakomboa wananchi wa Zanzibar kutoka kwa Wakoloni.

“Udumisheni utamaduni huu kwani unaleta mshikamano na furaha miongoni mwenu na ni njia nzuri ya kudhihirisha utamaduni wetu kwani Zanzibar watu wake ni wavuvui kihistoria” alisema Mwadini

Alifahamisha kuwa kuudumisha mchezo huo ni kuwapa umuhimu Wavuvi ilikuona na wao wanathaminiwa na taifa lao kwavile viongozi wa Serikali ndio wanaokuwa Wageni rasmi na Wadhamini wa mchezo huo.

 Waziri Mwadini aliwaomba Washriki wa mchezo huo kuwahamasisha wenzao kutoka Vitongoji mbalimbali vya Zanzibar kushiriki mchezo huo ili kuunogesha zaidi.

Aidha aliwataka pia Washirikia kujiandaa vyema zaidi katika mashindano yanayokuja na kuuthamini mchezo wao huo ambao amedai kuwa hauna tofauti na michezo mingine inayochezwa Zanzibar  

Mchezo huo ulishirikisha ngalawa 10 kutoka vitongoji mbali mbali vya unguja kama vile Dimani ,chukwani ,Nyamazi Bumbwni ambapo Mshindi wa mchezo huo Fundi Abubakari kutoka Bubwini alizawadiwa Shilingi Laki 2.

 

 IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR  11/01/2012

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.