Rais wa Zanzibar na mwenyekiti Baraza la Mapinduzi Dr,Ali Mohd Shein akifanya uzinduzi rasmi wa jengo jipya la kurushia matangazo kupitia mfumo wa Digital lililopo Raha leo mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti Baraza la Mapinduzi Dr,Ali Mohd Shein akifanya uzinduzi rasmi wa jengo jipya la kurushia matangazo kupitia mfumo wa Digital lililopo Raha leo mjini Unguja

 

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi ameitaka wizara ya Habari utamaduni utalii na Michezo kutoa ufafanuzi kwa raiya kuhusiana na suala zima la matangazo kupitia mfumo mpya wa Digital kutokana na jamii kutokua na uelewa juu ya mfumo huo mpya.

 

Dk:Shein ameyasema hayo wakati alipokua akizindua rasmi  ufunguzi  wa mradi mpya wa matangazo kupitia digital huko Rahaleo wilaya ya mjini unguja.

 

Dk;Shein amesema kuwa Jamii Nchini imekua ikijiuliza  maswali mengi juu ya mfumo  mpya wa matangazo unaozungumziwa hivi sasa pasipo na kuelewa chochote ,wana imani kwamba tv zao za zamani zitakuwa hazifai kutumiwa tena na wanunue tv mpya jambo ambalo sio sahihi,hivyo basi wanahitaji kuelimishwa ipasavyo kwa lengo kupata  ufahamu juu ya mfumo huo.

 

Sambamba na hayo,amelitaka shirika la habari  Zanzibar(ZBC)kufanya kazi ipasavyo ili kuenda sambamba na mahitaji ya wananchi na taifa kwa ujumla,kama yalivo mashirika mengine ulimwengini,ameshangazwa na kuwa ZBC ilikuwa ndio tv ya mwanzo ya rangi Afika mashariki  lakini sasa imekua ndio ya mwisho kutokana na utendaji wake.

 

Pia amezibainisha  baadhi ya changamoto zinazolikabili shirika hilo kua ni  pamoja na uendeshaji mbovu wa vipindi visivyo na mahitaji kwa jamii,pia amesema kumekuwa na tatizo la kuendesha vipindi vya habari kwa muda usio sahihi kama ilivopangwa.

 

Hivyo Dk;Shein , amemtaka  Waziri wa habari Utamaduni Utalii na michezo pamoja na Katibu wake kuhakikisha kua kazi inatendeka ipasavyo ili kulinda mahitaji ya wanachi kupitia ZBC.

Aidha amesema kuwa yeye amekuwa akiwachagua watu wenye sifa ili kuendesha shirika hilo lakini anashangazwa na maneno yanayosemwa na baadhi ya watu kuwa amekuwa akichagua rafiki zake lakini suala hilo sio sahihi kwani angemchagua mwanawe ambae pia kasomea masuala ya habari.

Sambamba na hayo ameiagiza wizara ya habari kuliangalia upya suala la kuwafungia wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar kwani vijana wamekuwa na makosa mengi hivyo basi si vyema kutumia jazba dhidi yao badala yake njia ya busara itumike na kumaliza tatizo hilo.

Jengo jipya la kurushia matangazo kupitia mfumo mpya wa digitali liliopo Rahaleo mjini Unguja
Jengo jipya la kurushia matangazo kupitia mfumo mpya wa digitali liliopo Rahaleo mjini Unguja

 

Raisi amezindua rasmi majengo mawili moja ni la kuendeshea matangazo ya Digital na moja ni kwa ajili ya studio mpya  ya kisasa yenye lengo la kurikodia filamu na muziki kwa wasanii wa Zanzibar

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.