Rais wa Zanzibar na mwenyekiti Baraza la Mapinduzi Dr,Ali Mohd Shein akifanya uzinduzi rasmi wa jengo jipya la kurushia matangazo kupitia mfumo wa Digital lililopo Raha leo mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti Baraza la Mapinduzi Dr,Ali Mohd Shein akifanya uzinduzi rasmi wa jengo jipya la kurushia matangazo kupitia mfumo wa Digital lililopo Raha leo mjini Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk, Ali Mohammed Shein amewataka wafanyakazi wa shirika la utangazaji Zanzibar ZBC kuongeza juhudi na ubunifu ndani ya  utendaji wa kazi zao ili kulifanya shirika hilo kukidhi viwango vya kitaifa na kimataifa.

Amesema kuwa kuongeza juhudi na ubunifu wa vipindi mbalimbali vyenye kutoa elimu na kuburudisha vinavyo kwenda na wakati kutalisaidia shirika hilo kuenda sambamba na madiliko ya sayansi na teknolojia yanayo endelea ulimwenguni.

Dk, Shein ameyaeleza hayo wakati akizindua mradi wa miundombinu ya utangazaji katika mfumo wa Digital na studio za kisasa za kurekodia sannaa na muziki huko Rahaleo mjini Zanzibar.

Amesema kuwa Zanzibar kama zilivyo nchi nyengine duniani imeamua kubadisha mfumo wa matangazo kutoka analogue kwenda Digital ili kuendana mabadiliko ya ulimwengu hivyo ni muhimu kwa watendaji wa shirika hilo kufanya kazi kwa bidii ili kuendana na mabadiliko hayo.

Pia ameelezea kusikitishwa kwake na utendaji usioridhisha wa shirika hilo kutokana kutoonekana vizuri kwa ZBC TV na kutokusikika vizuri kwa matangazo ya Radio kutokana sababu zinazoweza kuepukika.

Dk, Shein alisema kuwa serikali ya mapinduzi Zanzibar haitovumilia kuona utendaji mbovu wa shirika hilo kutokana na sababu zinazoweza kuepukika hivyo ameiagiza wizara ya habari kusimamia vyema utendaji wa shirika hilo ili kuondokana matatizo yaliopo.

“Serikali haitovumilia tena kuona utendaji mbovu katika sekta ya utangazaji kutokana na kuwepo kwa ubora wa mindo mbinu ya utangazaji hapa Zanzibar.” Alisema Dk, Shein

Akizungumzia kuhusu Studio ya kurekodia Sanaa na Muziki Dk, Shein amesema kuwa kuzinduliwa kwa studio hiyo kutawawezesha wasanii kuimarisha vipaji vyao hatua ambayo itaongeza kipato chao pamoja na kuondokana na adha ya kutafuta studio zisizo na viwango jambo linalo pelekea kukosa ubora wa kazi zao.

Pia amewataka wasanii kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili na silka za Wazanzibari na kuepukana na upotoshaji wa jamii kupitia kazi zao,akizungumzia kuhusu suala la kufungiwa kwa wachezaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar ameitaka wizara husika kuangalia njia mbadala ya kulitatua tatizo hilo na sio kuamua tu kwa kutumia jazba,

Nae Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mh, Said Ali Mbarouk amesema kuwa kuchelewa kukamilika kwa miundo mbinu ya mfumo Digital hapa Zanzibar kunatokana kuzingatia ubora wa miundo mbinu hiyo kutokana na mabadiko yatakayo weza kutokea ili kupunguza gharama kwa Serikali na Wananchi.

Pia amesema kuwa Wizara yake tayari imeandaa utaratibu maalum wa upatikanaji wa ving’amuzi ambavyo vitaanza kuuzwa mwishoni mwa mwezi huu katika vituo mbalimbali Unguja na Pemba ambavyo vitatangazwa hapo baadae kwa gharama ya shilingi 50000 kwa kila king’amuzi kimoja.

Aidha amesema kuwa vuing’amuzi vitakavyo uzwa vitakua na ubora wa hali ya juu kulinganisha na ving’amuzi vyengine kutokana na kuwa na huduma mbalimbali zikiwemo Internet, pamoja mawasiliano ya makundi maalum.

Jumla ya shilingi bilioni nane zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa jingo la miundo mbinu ya mfumo wa Digital na matengenezo ya jingo la studio za kurekodia kazi za wasanii fedha ambazo zimetolewa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Uzinduzi huu unakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika mwaka 1964

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.