Vodacom wakitoa Msaada picha sio halisi ya tukio la Pemba
Vodacom wakitoa Msaada picha sio halisi ya tukio la Pemba

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom imetoa msaada vyakula na vitu vingine kwa vituo vinne vya kusadia watumiaji wa dawa za kulevya kuachana na dawa hizo (sober House) vilivyopo kisiwani Pemba.

Katika ziara hiyo ambayo ilimjumuisha Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, kampuni hiyo mbali na kutoa msada wa vyakula ilitoa dawa za kusafishia vyoo, sabuni.

Akizungumza mwishoni mwa wiki katika vituo kilichopo Chakechake, Profesa Mbarawa, aliwataka vijana kuhakikisha matumaini waliyoyaonesha ya kutaka kuachana na matumzi ya dawa hizo hayapotei.

Alisema uamuzi waliouchukua wa kutaka kuachana na matumizi ya dawa hizo ni wa msingi na unawawezesha kurudi katika maisha yao ya kawaida sanjari na kutimiza ndoto za maisha walizokuwa nazo.

“Nimejulishwa kwamba kuingia katika nyumba hii ni lazima mtumiaji mwenyewe ukubali kuwa yupo tayari kuachana na dawa za kulevya. Hilo ni jambo jema na linalonyesha mnayo matumaini ya kurudi katika maisha ya kawaida ,” alisema.

Aidha, alieleza kuwa serikali imekuwa ikifanya juhudi kukomesha biashara hiyo na kwamba hata mawaziri wameshawahi kuoneshwa mikanda ya video inayoonesha athari za dawa za kulevya.

Awali, Meneja wa Vodacom Foundation, Grace Lyon alisema kampuni hiyo imefika katika nyumba hizo ikitekeleza kwa vitendo dira yake ya kusaidia makundi yenye uhitiji kupitia programu ya ‘Pamoja na Vodacom’ inayotekelezwa kwa michango ya wafanyakazi na kampuni.

“Tatizo la dawa za kulevya sio la mtu mmoja linatugusa sote kama sio ndani ya familia basi kuna ndugu, jirani au hata rafik. Wito wangu mkubwa ni kuwaomba kujitahidi kuhakikisha hamrudii kutumia dawa hizi,” alisema.

Kwa upande wake, Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom, Salum Mwalim, alipongeza utayari wa viijana hao kuachana na matumizi ya dawa hizo.

CHANZO TANZANIA DAIMA

2 thoughts on “Vodacom yasaidia Sober House Pemba”

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.