Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akitoa hotuba yake ya uzinduzi wa mradi wa E-Government Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi.

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amezindua rasmi mfumo wa mawasiliano ya kiteknolojia wa serikali yake, ambapo shughuli zote za serikali zitaweza kuratibiwa na kufahamika kwa njia ya mtandao.  Sherehe za uzinduzi wa mradi huo zimefanyika Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema lengo la Mradi wa E-Government ni kuiwezesha Serikali kuendesha shughuli zake kwa njia za kitaalamu zaidi na kuhakikisha kuwa kila mwananchi popote alipo anapata huduma au taarifa muhimu zinazotolewa na Serikali kupitia mitandao mbalimbali itakayokuwa karibu naye.

Ameongeza kuwa Mradi huo utaisaidia sana Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kufanya kazi zake kwa ufanisi mkubwa na kwa haraka katika kukabiliana na kasi ya mabadiliko ya kilimwengu kama yanavyoshamiri siku hadi siku duniani.

“Ni jambo la fahari sana kuwa leo hii Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inajiunga rasmi na nchi zingine duniani katika mfumo mpya wa uendeshaji wa shughuli za kiserikali ujulikanao kama E-Government” alisema Shein.

Ameongeza kuwa Mradi huo pia utakuwa ni kichocheo muhimu katika kuendeleza dhamira ya Serikali ya kukuza matumizi ya Teknologia ya habari na Mawasilino nchini.

Afisa Usalama wa Mradi wa E-Governmet Ali Mohamed Khitu akimfahamisha Rais Shein mchoro unaoonesha jinsi Waya wa Mradi huo ulivyosambazwa katika Visiwa vya Unguja na Pemba na kuwawezesha kugundua uharibifu popote pale utakapotokea.

Amezitaja baadhi ya faida za Serikali Mtandao kuwa ni pamoja na kukuza Elimu katika Skuli za Msingi na Sekondari kwa kupitia Mradi wa T21, ili kukabiliana na mabadiliko yanayoikumba sekta ya habari na mawasiliano.

Aidha Dkt. Shein amefahamisha kuwa Mradi huo pia unaweza kuipunguzia gharama Serikali ya kusafirisha wagonjwa nje ya nchi kwa matibabu ambapo Madaktari wa ndani wanaweza kuunganishwa na madaktaari waliopo nje ya nchi na kuweza kusaidiana kuwafanyia Operesheni wagonjwa waliopo Zanzibar.

Dkt Shein pia amefahamisha kuwa Mradi huo utatoa fursa nzuri kwa wafanyabiashara na wawekezaji nchini katika kundesha biashara zao ikiwa ni pamoja na kujtangaza,kutafuta masoko na kutoa huduma bora kwa wateja wao.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais utumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar Kheri amesema Taasisi za Kiserikali zitaunganishwa katika utendaji na uendeshaji wa shughuli zao kwa njia za uhakika,salama na kwa uharaka.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein wa katikati waliokaa katika picha ya pamoja na Maofisa mbali mbali katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa E-Government ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi

Aidha amewataka wananchi kuiheshimu miundombinu ya mradi huo ili uweze kuwa endelevu kwa manaufaa ya wananchi wote.

Akitoa salam zake Balozi wa Watu wa China nchini Tanzania Lu Youqing ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mashirikiano ambayo imekuwa ikitoa kwa nchi ya China katika kuendeleza mahusiano ya nchi husika.

Aidha ameahidi kuzidisha mashirikiano na Zanzibar katika kusaidia wananchi wake kukabiliana na changamoto za maisha hasa katika sekta ya uchumi,elimu na Afya.

Mradi wa Serikali mtandao E-Government ambao umezinduliwa ikiwa ni shamra shamra za Sherehe za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar umeigharimu Dola Milion 19 za kimarekani ambazo ni Mkopo nafuu kutoka nchi ya China.

IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.